Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Maafisa Uhamiaji katika Kiwanja cha Ndege Cha Kimataifa
Cha Julius Nyerere(Terminal II), alipotembelea kuangalia utendaji kazi
na vifaa vya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka
hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka
hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa
malekezo wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) Mhandisi George Sambali (Katikati), alipotembelea Mamlaka
hiyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza
na Mawakala wanaofanya kazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA),alipotembelea kuona utendaji kazi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Swissport, Gaudence Temu, wakati
alipotembelea Ofisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza
jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
hawapo pichani, wakati alipoongea nao jijini Dar es Salaam.
(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)
WAZIRI MBARAWA AIAGIZA TAA KUONGEZA MAPATO.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiagiza
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuongeza kiwango cha
ukusanyaji mapato kutoka Bilioni 74 hadi kufikia bilioni 105 katika
mwaka wa fedha 2016/2017.
Ametoa
agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyakazi wa
Mamlaka hiyo mara baada ya kukagua majengo matatu na ofisi mbalimbali
zilizopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
Amesisistiza
wafanyakazi wa Uwanja huo kuhakikisha kiasi cha ukusanyaji wa mapato
hayo kinaongezeka siku hadi siku ili kukuza uchumi wa taifa na kuchochea
fursa za kimaendeleo.
“Ni
lazima muongeze kasi ya kufanya kazi ili mapato yaongezeke kwa kuwa
uwezo mnao na nimeona kwenye viwanja vyenu kuna sehemu nyingi za
biashara, hivyo mna kila sababu ya kukusanya kiasi hicho cha fedha”,
amesema Prof. Mbarawa.
Aidha,
katika ziara hiyo Waziri Prof. Mbarawa alibaini ucheleweshwaji wa
vibali kwa abiria wanaoingia katika Uwanja wa Ndege wa JNIA ambapo
abiria huchukua zaidi ya saa moja kupata vibali.
“Nimesikitishwa
na kitendo cha ucheleweshwaji wa vibali kutoka Idara ya Uhamiaji na
huduma za kibenki zinazotolewa… hali hii haileti picha nzuri kwa wageni
wetu. Abiria kuwekwa zaidi ya saa moja akisubiri kupata huduma, sitaki
kuona hali hiyo ikiendelea”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Sambamba
na hilo amezitaka taasisi zote zinazofanya kazi katika viwanja vya
ndege kushirikiana kwa ukaribu ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa
huduma na kuongeza mapato kwa taifa.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Eng. George Sambali
amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mapungufu yaliyobainishwa
yatafanyiwa kazi ili kuongeza ufanisi na huduma bora kwa abiria.
“Kwa
kushirikiana na taasisi zote ambazo zinafanya kazi katika Kiwanja hiki
tutahakikisha tunatoa huduma nzuri na kuongeza ufanisi katika utendaji
ili kufikia malengo”, amesema Eng. Sambali.
Waziri
Prof. Mbarawa amefanya ziara ya siku moja katika Kiwanja cha JNIA ili
kuona utendaji kazi na maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria
ambapo jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2017 na litakuwa
na uwezo wa kuhudumia zaidi ya abiria milioni sita kwa mwaka.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano .
No comments:
Post a Comment