Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
Askari na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza
alipofanya ziara mkoani humo kwa lengo la kujua jinsi Jeshi hilo
linavyofanyakazi mkoani humo. Masauni katika hotuba yake aliwataka
viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa
sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na
watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu
Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu
Nguya akitoa maelezo ya utendaji kazi wa Jeshi lake mkoani humo kwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia).
Masauni katika hotuba yake aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye
kazi kwa kujituma zaidi na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati
wanapoenda katika matukio ya uzimaji moto na watakaofanya hivyo
watachukuliwa hatua kali. Kushoto ni Mratibu Msaidizi wa Jeshi hilo,
Mussa Kaboni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
Kaunda suti) akiangalia jinsi askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
wanapokuwa wanazima moto katika matukio mbalimbali. Kulia ni Kaimu
Kamishna wa Jeshi hilo Mkoa wa Mwanza, ACF Hamidu Nguya. Masauni
alifanya ziara katika Ofisi za Jeshi hilo jijini Mwanza kwa lengo la
kujua jinsi gani jeshi hilo linavyofanyakazi mkoani humo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kuzungumza na Askari na
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza. Masauni
aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi na
waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya
uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akiwasalimia Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wa Mkoa wa Mwanza
wakati alipokuwa anawasili katika ofisi za Jeshi hilo, jijini Mwanza.
Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi
na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya
uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa
Kaunda suti), Kaimu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa
Mwanza, ACF Hamidu Nguya (wanne kulia) na akiwa katika picha ya pamoja
na Maafisa wa Jeshi hilo mkoani humo. Masauni alifanya ziara katika
ofisi za Jeshi hilo kwa lengo la kujua jinsi gani jeshi hilo
linavyofanyakazi katika matukio mbalimbali jijini Mwanza. Hata hivyo,
Masauni aliwataka viongozi wa jeshi hilo wafanye kazi kwa kujituma zaidi
na waepuke kutoa sababu za kizembe wakati wanapoenda katika matukio ya
uzimaji moto na watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment