Matukio : VETA yang'ara Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Jul 2016

Matukio : VETA yang'ara Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar

Rais wa Rwanda, Paul Kagame akiwana mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli (wakwanza kulia) amkiwakabidhi tuzo Mkurugenzi wa Kanda wa Chuo cha VETA, Habibu Bukko(Kushoto) katika maonesho ya 40 ya kibiashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wageni waliotembelea katika banda la VETA wakisaini kitabu cha ushiriki katika maonesho ya 40 ya kimataifa ya mwaka huu katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Technolojia na ufundi, Mhandisi Stella Manyanya akipewa maelekezo na  Meneja wa Mawasiliano  VETA, Peter Sitta alipotembelea banda la VETA katika maonesho ya 40 ya kimataifa jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Masomo yanayofundishwa na chuo cha VETA katika maonesho ya kimataifa ya 40 katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Wananchi wakiwaangalia Bustani inayohifadhi mazingira hasa kwa wakazi wasio na maeneo makubwa kwaajili ya Kulima Bustani (Vertical Garden) ambayo huoneshwa na banda la VETA jijini Dar es Salaam leo. 
 Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo katika banda la VETA kitengo cha vitu vya Samani katika maonesho ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo walipotembelea banda la VETA kitengo cha Umeme katika maonesho ya 40 ya kibiashara ya kimataifa katika viwanja va sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
 Meneja wa Mawasiliano  VETA, Peter Sitta akijadiliana jambo  mtaalaam mamlaka ya VETA leo  katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimatiafa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mzazi kulia na mtoto aliyekaa kwenye kiti wakipata maelekezo walipotembelea banda la VETA kitengo cha Vitu vya Samani jijini Dar es Salaam leo.
 Wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mkufunzi wa Viatu vya Ngozi ambavyo hutengenezwa katika chuo cha ufundi stadi cha VETA katika maonesho ya 40 ya kibiashara ya kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wananchi wakipata  maelezo juu ya ufundi umeme walipotembelea banda la VETA katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimatiafa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakipata maelekezo juu mitaala ya VETA walipotembelea  banda hilo  katika maonesho ya 40 ya biashara ya kimatiafa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Post Top Ad