Matukio : Elimu ya juu nchini Kuchukua Sura Mpya - Naibu Waziri Jaffo - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


10 Jul 2016

Matukio : Elimu ya juu nchini Kuchukua Sura Mpya - Naibu Waziri Jaffo


 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo amesema kuwa fursa za elimu ni nyingi katika vyuo vya nje ya nchi na gharama zake ni nafuu.

Jaffo ameyasema hayo wakati wa maonesho ya biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere (Sabasaba) katika banda la Global Education Link (GEL), amewataka Watanzania kutumia maonyesho ya Sabasaba kuwa ni kipindi muafaka kupata mambo mengi kwa wakati mmoja likiwamo suala la elimu katika vyuo vya nje.

Jaffo amesema kuwa, maonesho ya sabasaba ni kipindi pekee kwa taasisi mbalimbali na huduma zake zinatolewa bure.Aidha amesema kuwa wazazi wanaotaka kuwasomesha watoto wao katika vyuo vya nje ya nchi kwa gharama nafuu watumie fursa hiyo kupita katika banda la Global Education Link (GEL) watapata taarifa mbalimbali.

‘’Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imejipanga hivyo kama wasaidizi wake lazima tujipange kuhakikisha kwamba tuangalie jinsi ya kubadilika kwa kasi na kubadilika huko kwa kwa kasi lazima tuhakikishe tuna teknolojia yakutosha kabisa kwanza kiushindani, tuanzishe vitu ambavyo vitakuwa na soko kubwa”amesema .
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education link (GEL), Abdulmalik S.Mollel amesema kuwa vijana wanaopitia kampuni yao hata baada ya kupata udahili na kwenda masomoni nje ya nchi, wana utaratibu wa kufuatiliwa maendeleo yao ili mzazi aweze kuona thamani ya fedha anayetoa kwa kusomesha mtoto nje ya nchi.

Mollel amesema kuwa vyuo vya nje wanavyokwenda wanafunzi kuna wawakilishi wanaofanya kazi moja kwa moja na GEL ya kufatilia mienendo ya wanafunzi wao kwa kipindi chote wanachosoma na taarifa zao zinatumwa na kisha mzazi kupewa taarifa za maendeleo ya mtoto.

Amesema kuwa watoto wanaokwenda kusoma vyuo vya nje vinatambuliwa na TCU na vinatambuliwa na bodi za nchi husika ili kuweza kumsaidia mtoto kuwa na uhakika wa elimu na utaalam aliyopata katika vyuo hivyo.

Global Education Link (GEL) inaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa mzazi anaweza kumudu gharama hizo na hakuna tofauti na vyuo vya ndani.Anasema mtoto anayesoma nje wanaangaliwa kwa kila namna kuanzia ili kumuondolea mzazi usumbufu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education link (GEL), Abdulmalik S.Mollel  akizungumza jambo na  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemain Jaffo alipokuwa akiagana nae mara baada ya kulitembelea banda hilo
 Baadhi ya Wadau mbalimbali wakiingia na kutoka ndani ya Banda hilio.

KUTOKANA na uhitaji wa utaalam katika nchi katika kuelekea uchumi wa kati vijana wanatakiwa kupata ujuzi na masomo hata katika vyuo vya nje.


Aliongeza kuwa kuna fursa nyingi sio kwa serikali peke yake lakini hata kwa wazazi wenyewe kutumia fedha zao kwa mambo ya msingi kuliko kufanya harusi ya Sh. milioni 50 au milioni 100.Amesema sh.milioni 50 zinazotumika katika harusi zinaweza kuziwekeza kwa vijana wetu katika kuwapatia elimu iliyo bora zaidi kwa ajili ya uchumi wa nchi yetu tunaweza kufanya vizuri zaidi.

Jaffo amesema kuwa udahili wa wanafunzi katika vyuo vya ndani katika uhandisi, Udaktari wa Binadamu ni chache kutokana na mfumuko wa ufaulu kwa kidato cha sita pamoja na stashahada hivyo wanaweza kusoma katika vyuo vya nje ambavyo vimeweza kuwekeza katika maeneo hayo.

“Leo hii nikwambie ndugu tembelea katika kila siku za mapumziko fanya tathmini kila harusi iliyopo inayofanywa na sisi wenyewe ndio tunatengeneza harusi, unajikuta kumbe tungekuwa na mpango mkakati mzuri wa kuhakikisha jinsi gani vijana wetu tunakuwa na wataalamu katika sekta ya gesi, madini, kilimo pamoja na viwanda vidogo vidogo kwani kwa miaka mitano wenzetu kutoka nchi mbali mbali watakuja kutuchukua".amesema Jaffo.




Mollel amesema kuwa watanzania kuondokana na fikra mgando kuwa wanaokwenda nje ni watoto wa mafisadi hakuna kitu hicho na tunatakiwa kuondokana dhana hiyo haitatusaidia kutokana serikali ilivyojipanga ya kuwa na wataalam katika nyanja mbalimbali.

Gharama ya kusoma nchini China ni milioni nane kwa kozi ya udaktari ambapo unaweza kusoma nchini katika vyuo vya binafsi.Watoto wanaokwenda kusoma vyuo vya nje vinatambuliwa na TCU na vinatambuliwa na bodi za nchi husika ili kuweza kumsaidia mtoto kuwa na uhakika wa elimu na utaalam aliyopata katika vyuo hivyo.

Global inaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa mzazi anaweza kumudu gharama hizo na hakuna tofauti na vyuo vya ndani kwa baadhi ya nchi.Anasema mtoto anayesoma nje wanaangaliwa kwa kila namna kuanzia ili kumuondolea mzazi usumbufu.

Mollel amesema kuwa watanzania kuondokana na fikra mgando kuwa wanaokwenda nje ni watoto wa mafisadi hakuna kitu hicho na tunatakiwa kuondokana dhana hiyo haitatusaidia kutokana serikali ilivyojipanga ya kuwa na wataalam katika Nyanja mbalimbali

Gharama ya kusoma nchini China ni milioni nane kwa kozi ya udaktari ambapo unaweza kusoma nchini katika vyuo vya binafsi.Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Profesa Lugano Kusiluka alisema kuwa GEL wanafanya kazi vizuri katika kufanya utaratibu wa vijana kutafuta vyuo vya kusoma ambavyo vinatambulika na TCU.

Amesema kuwa wanaona jinsi gani ya kushirikiana na GEL na Chuo cha Mzumbe katika eneo la vyuo vya nje ili kuweza kufika sehemu nzuri kwa kubadilishana uzoefu.Amesema naye alishakwenda kusoma nje hivyo ameshauri vijana kutambua nini wanaenda kufanya huku taifa likiwa linahitaji ujuzi wanaokwenda kuchukua.

Baadhi ya Wanafunzi waliosoma vyuo vya nje kwa kupitia GEL wamesema kuwa utaratibu ni mzuri katika kuandaa mazingira na mawasiliano na vyuo husika ambavyo wanakweda.Anita Ituwe ,amesema kuwa wakati alipokuwa anatafuta jinsi ya kupata vyuo vya nje walipata usumbufu lakini baada ya kufika GEL walipata maelezo ya kutosha na kuweza kujiunga katika chuo kimoja nchini India.

Amesema GEL wanaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa wazazi jinsi ya kumudu gharama za masomo katika vyo hivyo ambavyo vinaratibiwa na GEL.Amesema kuwa kuna mazingira bora ya kusoma vyuo vya nje kutokana uwekezaji kuwa kila kitu kinachohitajika kwa mwanafunzi kinapatikana ndani ya chuo bila kutoa gharama yeyote.

Nae Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Tanzania Taliki Abubakar ,amesema kwa wakati alipokuwa anatafuta chuo cha kusoma alikuwa hana uhakika lakini baada ya kukutana na GEL aliweza kupata Chuo cha kusoma na taratibu zilikwenda haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad