Na Anitha Jonas – MAELEZO
Watendaji wa Mkoa wa Pwani watakiwa kuwa wawazi kwa waandishi wa habari pale wanapotaka kupata taarifa kutoka kwao.
Hayo
yamesemwa leo Mjini Kibaha, Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipofanya ziara ya
kikazi mkoani hapo kufuatilia utekelezwaji wa maendeleo ya kisekta kwa
wizara yake.
“Kwa
kuwapa ushirikiano wakutosha waandishi wa habari kutasaidia kuepuka
kuandikwa kwa habari zisizona taarifa kamili ambazo huleta mkanganyiko
kwa jamii na kuharibu taswira ya ofisi, hivyo ni vyema mshirikiane
nao”,alisema Naibu Waziri Wambura.
Pamoja
na hayo Mhe. Naibu Waziri aliangiza kuwa katika bajeti ya mwaka
2016/2017 Kitengo cha Habari kipewe kipaumbele na kitengewe bajeti
itakayokidhi mahitaji pamoja na kununuliwa vitendea kazi ili kurahisisha
utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi ikiwa ni pamoja na kutangaza
shughuli za maendeleo ya Mkoa.
Kwa
upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw.Shangwe Twamala alisema mkoa
huo unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Maafisa Michezo kwa baadhi ya
Wilaya pamoja na Maafisa Utamaduni ila suala hilo kwasasa
limeshawasilishwa kwa ngazi husika na wanalifanyia kazi.
Pamoja
na hayo Kaimu wa Mkoa huyo aliendelea kusema Mkoa huo unakabiliwa pia
na changamoto ya usikivi wa matangazo ya Redio na Televisheni kwa baadhi
ya maeneo kama Rufiji,Mafia na mengineyo.
Naye
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya
Mashariki Bw.Bernard Haule alitoa ufafanuzi kuhusu suala la kukatwa kwa
matangazo katika chaneli zote pale malipo yanapoisha katika ving’amuzi
vya Azam na Zuku kwa kusema leseni zao ni tofauti na zile za Startimes
na Continental ambazo mbali na malipo ya kifurushi yanapokwisha wao bado
huonyesha chaneli tano za taifa bure ambazo ni ITV,Star Tv,Channel Ten,
EATV na TBC 1.
Pamoja
na hayo Mhe.Wambura aliagiza kuwa watendaji wahakikisheni wanatenga
maeneo ya viwanja vya michezo yasiyo na mgogoro kwani michezo ni ajira
na inasaidia vijana kujikwamua kiuchumi,hivyo ni vyema ipewe kipaumbele.
Halikadhalika
Naibu Waziri Wambura alitoa wito kwa wasanii Muziki wa Mkoa wa Pwani
kuiga mfano wa marehemu Baraka Mwishehe kwa kutunga nyimbo zenye maadili
na zenye kubeba ujumbe wa kuelimisha na kuburudisha jamii.
Hata
hivyo Naibu waziri aliendelea kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla
kuenzi lugha ya Kiswahili kama yanavyofanya mataifa mengine duniani
kuenzi lugha zao mfano China.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkoa Pwani (hawapo pichani) alipofanya ziara yake ya kikazi leo mkoani kwa lengo la kujua maendeleo ya kisekta kwa upande wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Kaimu Mkuu wa Mkoa Pwani Bw.Shangwe Twamala akitoa taarifa maendeleo ya kisekta kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (katikati) alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo leo Mjini Kibaha.
Afisa Tawala Wilaya ya Kibaha Bi. Sozy Mgate akieleza changamoto za sekta ya michezo kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara ya kikazi leo Mjini Kibaha kujionea maendeleo ya kisekta katika Mkoa huo.
Mwakilishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Mhandisi Christopher John akitoa ufafanuzi kuhusu kukosekana kwa usikivu wa matangazo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Mjini Kibaha,Mkoani Pwani kwa lengo la kujua maendeleo ya kisekta katika mkoa huo.
Mbunge wa Viti Maalum Pwani Mhe.Hawa Mchafu akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wapili kushoto) kwa kutembelea Mkoa wa Pwani leo na kujionea changamoto za kisekta zinazohusu Wizara yake.
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (watatu kushoto) alipofanya ziara ya kikazi Mjini Kibaha leo kujionea maendeleo ya sekta kwa wizara yake, (wapili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw.Shangwe Twamala na (wapili kulia) Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Hawa Mchafu.
Baadhi ya Maafisa Habari,Maafisa Michezo,Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (watatu kushoto) alipofanya ziara ya kikazi leo Mjini Kihaba,Mkoani Pwani kujua maendeleo ya sekta kwa wizara yake , (wapili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw.Shangwe Twamala na (wapili kulia) ni Mbunge wa Viti Maalum Pwani Mhe. Hawa Mchafu.
No comments:
Post a Comment