Timu
ya vijana chini ya umri 17 – Serengeti Boys, leo wamefanya ziara katika
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, ambao ni wadhamini wa
michuano ya vijana ya Airtel Rising Stars huku wakijiandaa na mechi ya
Kimataifa ya kufuzu kucheza fainali za Afcon 2017 itakayochezwa jijini
Dar es Salaam Jumapilihii.
Timu
hiyo inajumulisha wachezaji kumi waliochunguliwa kutoka katika michuano
iliyopita ya Airtel Rising Stars ambayo ilizinduliwa 2011 ikijumuisha
mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Akiongea
wakati wa ziara hiyo, Mkurungenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania
Beatrice Singano Mallya alisema kampuni inajivunia jinsi michuano ya
Airtel Rising Stars ilivyowapa vijana fursa ya kuonyesha vipaji vyao vya
soka na kupata nafasi ya kuchanguliwa kuchezea timu ya Taifa ya vijana.
Airtel
Tanzania inayo furaha ya kupewa nafasi ya kudhamini mpira Tanzania
kupitia michuano ya vijana ya kila mwaka ya Airtel Rising Stars.
Michuano hii ni moja ya mipango yetu ya kuwapa fursa vijana kupitia
kucheza mpira. Tunashukuru mpaka sasa hivi michuano hii imeweza kutoa
wachezaji kumi ambapo wanachezea timu yetu ya taifa ya vijana –
Serengeti Boys.
Wachezaji
hao ni Ramadhan Awamu (Golikipa), Shabaan Zuberi, Cyprian Benedict na
Ally Ng’anzi (Viungo), Mohammed Abdallah, Gadaffi Ramadhan na Nickson
Clement (Mabeki), Mohammed Abdallah, Dickson Job,Muhsim Malama na Yohana
Oscar (Washambuliaji).
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya soka la vijana kutoka
Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) Ayoub Nyenzi alisema ili timu
ya Taifa iweze kupata Mafanikio ni lazima kuwekeza kwenye miradi mbali
mbali ya kukuza soka la vijana huku akitoa Shukrani kwa kampuni ya
Airtel kuendeleza miradi huo kupitia Airtel Rising Stars.
Huu ni
mwaka wa sita mfululizo wa michuano hii ya Airtel Rising Stars. TFF
inatoa pongezi kwa Airtel kwa udhamini huu ambao umeweza kuwapa vijana
wengi fursa ya kutambua uwezo wao, alisema Nyenzi.
Michuano
wa Airtel Rising Stars awamu ya sita itazinduliwa Jumapili ya Juni 26
huku Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa mngeni rasmi.
Uzinduzi huo pia utahudhuriwa na wadau wengine wa soka nchini wakimemo
viongozi wa klabu, TFF, wachezaji wa zamani wa Airtel Rising Stars na
waandishi wa habari.
Mwenyekiti
wa kamati ya maendeleo wa soka la vijana Ayou Nyenzi akiongea na
wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka U-17
Serengeti Boys wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel Makao makuu jijini
Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Kocha
wa Serengeti Boys Bakari Shime akiongea na wachezaji wakati timu hiyo
ilipotembelea Airtel Makao makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Mkurugenzi
wa ufundi wa kamati ya maendeleo ya soka la vijana Kim Poulsen akiongea
na wachezaji wa Serengeti Boys wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel
Makao makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiwapungia mkono
wachezaji wa Serengeti Boys wakati timu hiyo ilipotembelea Airtel Makao
makuu jijini Dar es Salaam Juni 24, 2016.
Mmoja kati ya wachezaji wa Serengeti Boys akiongea wakati timu hiyo ilipotembelea ofisi za Airtel makao makuu.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano akiwa katika picha
ya pamoja na wachezaji wa Serengeti boya ambao wametokana na program ya
Airtel Rising Stars.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano na Mwenyekiti wa
kamati ya maendeleo wa soka la vijana Ayou Nyenzi (katika) wakiwa katika
picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka
17 Serengeti boys pamoja na viongozi wao wakati walipotembelea ofisi za
Airtel Makao Makuu Morocco jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment