Matukio : RITA yaadhimisha miaka kumi (10) na kilele cha wiki ya Utumishi - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


25 Jun 2016

Matukio : RITA yaadhimisha miaka kumi (10) na kilele cha wiki ya Utumishi


Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeadhimisha Miaka 10 tangu kuanzishwa pamoja na Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma hapo jana tarehe 23 Juni 2016.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson (wa tatu kutoka Kushoto) akimbemba mmoja wa Watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam  siku ya Maadhimisho ya Miaka Kumi ya kuanzishwa Wakala wa RITA. Watoto hao walisajiliwa na kupata Vyeti vya kuzaliwa hapo hapo Hospitali.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson akikabidhi Cheti Cha Kuzaliwa kwa Mama wa Mtoto.
 Mwananchi akipata maelezo kuhusu Masuala ya Mirathi na Wosia kutoka kwa Watumishi wa RITA.
 Bw. August Mbuya (katikati) akitoa maelezo na kupokea Kero kuhusu huduma za Wakala wa RITA  katika Dawati Maalumu.
1)      Kusajili na kutoa Vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wote waliozaliwa siku ya Tarehe 23 Juni 2016 katika Hospitali ya Amana jijini Dar Es Salaam. Pia Elimu kuhusu Huduma za Wakala kwa wananchi katika eneo hilo.

2)      Kuanzisha Dawati maalumu katika Ofisi ya Makao Makuu ya RITA kwa ajili ya kupokea Malalamiko, maoni, kero za Wananchi. Pia Dawati hilo limetoa Elimu kwa wananchi kuhusu huduma za Wakala.

3)      Kutoa Elimu kwa Umma kwa Wananchi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya Siku ya Wajane Duniani.

RITA inawashukuru Wadau wote walioshirikiana na Wakala katika kipindi cha Miaka Kumi (10) iliyopita.

Post Top Ad