Na Jonas Kamaleki
Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 11,820.503 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 11,820.503 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Philip Mpango wakati akitoa hotuba kuhusu taarifa ya hali ya uchumi
nchini na mpango wa maendeleo wa taifa 2016/17.
Waziri
Mpango amesema kuwa kiwango hicho ni sawa na asilimia 40 ya bajeti yote
ya serikali na kuongeza kuwa fedha za ndani ni shilingi bilioni
8,702.697 ambazo ni sawa na asiliia 74 ya bajeti ya maendeleo na fedha
za nje ni shilingi bilioni 3,117.805 sawa na aslimia 26 ya maendeleo.
Aidha,
Mpango amesema kuwa sekta binafsi inatarajiwa kuwekeza kiwango kikubwa
cha fedha ili kuanzisha na kuendeleza viwanda ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Mpango huo.
“
Kwa ujumla fedha za maendeleo zimeelekezwa zaidi katika miradi
inayolenga kuendeleza viwanda kama vile uchukuzi,ujenzi, nishati,
kilimo, maji, elimu na afya,”amesema Waziri Mpango.
Ameongeza
kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 umeainisha miradi
mikubwa ya kielelezo ambayo itapewa msisitizo katika utekelezaji wake.
Waziri
Mpango ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa makaa ya mawe ya
Mchuchuma, mradi wa chuma Liganga, ujenzi wa reli mpya kati ya Dar –
Kigoma na Tabora- Mwanza na matawi yake Isaka- Kigali/Keza- Msongati na
Kaliua- Mpanda kwa kiwango cha standard gauge.
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 utategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt Phillip Mpango akiwasilisha bungeni Hali ya
Uchumi wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwelekeo wa Mpango wa
Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Shally
Raymound (kulia) na Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge mjini
Dodoma Juni 8, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishina Valentino Mlowola
kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2016.
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Zamaradi Kawawa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 8,
2016.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Wabunge wa Viti Maalum (CCM) wakiongozwa na Mhe. Margaret Sitta wakijadili jambo nje
ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi cha bunge hilo.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Hamad Masauni katikati na Mbunge wa Kilolo
(CCM) Mhe. Venance Mwamoto wakiingia ndani ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma
kuanza kikao cha asubuhi cha Bunge.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiingia katika
viwanja vya Bunge kuanza kikao cha asubuhi cha Bunge hilo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye (katikati) pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakiwa katika picha ya
pamoja na mwanamitindo Tausi Likokola nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Phillip Mpango mara baada ya kuwasilisha hotuba ya taaarifa ya hali ya uchumi 2015
na mpango wa maendeleo wa taifa 2016/17 mjini Dodoma .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akibadilishana mawazo na
Wabunge wa CCM kutoka kushoto, Mhe. Mohammed Mchengerwa (Rufiji), Mhe. Vrajilal
Jituson (Babati Vijijini) na Mhe. Daniel Nsanzungwanko (Kasulu) mara baada ya kumalizika
kwa kipindi cha asubuhi.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati na
Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha asubuhi
cha Bunge linaloendelea mjini Dodoma. Kulia ni Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)
No comments:
Post a Comment