Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiendesha mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani (SDGs) kwa nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma kwa wanafunzi wa vitivo mbalimbali na walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyomalizika jana chuoni hapo.
Ninajisikia kuelimika na kuelewa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kiasi ya kwamba ninaweza sasa kuwaelimisha marafiki, vijana wenzangu na familia. Elimu hii hapo awali sikuwa nayo, sikuwa naelewa vyema malengo haya. Ukomo wa mpango huu wa dunia ni mwaka 2030 wakati ambapo mimi nitakuwa na umri wa miaka 40. Nataka kuwa sehemu ya mashuhuda wa mafanikio katika utekelezaji wake na ndio maana nataka kutimiza wajibu wangu kwa kupeleka elimu hii kwa wengine.” anasema Jane, mmoja wa washiriki wa semina.
VIJANA
1000 na wanazuoni 200 wa Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) wamepatiwa mafunzo ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani kwa nia ya kuwawezesha kutumia
maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma.
Kazi
ya kufunza malengo hayo ilifanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa
yaliyopo hapa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mhadhiri
Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Muya Said akitoa maoni wakati
wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu Duniani
(SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia
maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa
na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni
hapo.
Mafunzo
hayo ni sehemu ya juhudi ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwezesha uelewa kwa
tumaini kuwafanya wananchi hasa vijana kutambua wajibu wao katika
kutekeleza malengo hayo.
Mafunzo
hayo katika Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ni mwendelezo wa mafunzo
yaliyozinduliwa Arusha wiki iliyopita na Mratibu wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez.
Mafunzo
hayo yalifanywa kwa kundi la vijana 50 kutoka maeneo mbalimbali nchini
Tanzania ili waende kusambaza uelewa wa malengo hayo kwa vijana wenzao
nchini kote.
Mwanafunzi
wa Digrii ya kwanza ya Mifumo ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dodoma
(UDOM), Janeth Dutu akiuliza swali kwa mkufunzi wa mafunzo hayo (hayupo
pichani) wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya
kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa
Dodoma ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini
na kumalizika jana chuoni hapo.
Inatarajiwa kuwa zaidi ya vijana elfu 20 watakuwa wamepatiwa mafunzo katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Akizungumza
katika kampasi ya UDOM Bw. Rodriguez alisema kwamba Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDGs) yanahitaji ushirikiano wa watu wote ili
kuyafanikisha kama ilivyokusudiwa. Malengo ya Maendeleo Endelevu ukomo
wake ni mwaka 2030.
Aliwapongeza
wanachuo na wanazuoni kwa kujikita kwao kuelewa Malengo ya Maendeleo
Endelevu ambayo ndiyo malengo ya dunia ili kuweza kuyasimamia na
kuyatekeleza.
Pia
alizungumzia umuhimu wa vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo
hasa kwa kuzingatia kwamba asilimia 60 ya wananchi wa Tanzania ni
vijana.
“Mna
wajibu mkubwa kwa vijana wenzenu” alisema Bw. Rodriguez na kueleza
kwamba amefurahishwa kuona kwamba vijana na wanazuoni 1,200 wameahidi
kuwa walimu na mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu majumbani kwao,
katika taasisi zao na katika jamii inayowazunguka.
Pichani
juu na chini ni Sehemu ya wanafunzi na walimu wa UDOM wakimsikiliza
mkufunzi Hoyce Temu (hayupo pichani) kwa makini wakati wa mafunzo ya
siku mbili yaliyomalizika jana chuoni hapo.
Alisema
katika hilo Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kuhakikisha kwamba
wake kwa waume na vijana wanatekeleza wajibu wao kwa kushiriki vyema
katika mipango ya maendeleo yenye kulenga kufanikisha Malengo ya
Maendeleo Endelevu duniani.
Alisema wajibu wa kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu duniani kunategemea watu wote na hasa vijana.
Akipongeza
juhudi za kuelimisha za Umoja wa Mataifa, Profesa Flora Fabian kutoka
UDOM, alisema chuo hicho kimefurahishwa kuwa moja ya vituo vya kufunza
mabalozi vijana wa kusambaza elimu na wajibu katika kufanikisha Malengo
ya Maendeleo Endelevu.
Alisema
malengo hayo ya Dunia ni lazima yajulikane kwa kila mmoja; huku
akiwataka wanazuoni kuyazungumza katika kazi zao za kila siku, katika
tafiti na ripoti kama ilivyo kwa wanafunzi ambao wanastahili kupikwa
kuwa katika nafasi ya kuweza kuchambua malengo hayo kwa kuwa na takwimu
na taarifa sahihi.
Alipongeza
uamuzi wa utoaji elimu wa Umoja wa Mataifa na kuamini kwamba
watasambaza elimu hiyo kwa vyuo vikuu vyote nchini Tanzania.
Septemba
2015, viongozi kutoka nchi 193 duniani walitia saini Malengo ya
Maendeleo Endelevu duniani. Malengo hayo mapya yanatarajiwa kufanyiwa
kazi katika kipindi cha miaka 15 huku ikiweka pamoja shughuli za
maendeleo ya kijamii, kiuchumi yanayojali mazingira kwa ajili ya kizazi
cha sasa na kijacho.
Mmoja wa wanafunzi wa UDOM akipitia makabrasha ya SDGs wakati wa mafunzo hayo.
Mkufunzi
wa mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs), Hoyce Temu
akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo wakati zoezi la maswali
na majibu.
Mhadhiri
Msaidizi wa Maendelelo ya Jamii katika Chuo cha Sayansi za Jamii, Sanaa
na Lugha (CHSS) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Angelo Shimbi
akitoa maoni wakati wa mafunzo ya siku mbili ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yenye nia ya
kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa
Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini na
kumalizika jana chuoni hapo.
Beatrice
Mkiramweni kutoka Ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini, akipitia makabrasha ya SDGs wakati wa mafunzo ya siku mbili ya
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa
UDOM yenye nia ya kuwawezesha kutumia maarifa yake kusukuma mbele
maendeleo ya mkoa wa Dodoma yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa
Mataifa nchini na kumalizika jana chuoni hapo.
Mafunzo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia (SDGs) kwa wanafunzi na walimu wa UDOM yakiendelea chuoni hapo.
Kutoka
kushoto ni Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Development Studies -UDOM,
Edson Baradyana, Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi
ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa, Mtaalamu
wa Upangaji na Usimamizi wa Miradi -PRO UDOM, Radhia Rajabu, Mhitimu wa
kidato cha sita, Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa
Tanzania (YUNA) katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP),
Alvaro Rodriguez.
Kutoka
kushoto ni Mtaalamu wa mawasiliano katika Ofisi ya Mratibu wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu, Mhitimu wa kidato cha sita,
Aisha Msantu wa Asasi ya Vijana wa Umoja Taifa Tanzania (YUNA) pamoja na
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa katika picha ya ukumbusho
mara baada ya kuhitimisha mafunzo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki kwenye mafunzo ya SDGs yaliyomalizika jana chuoni hapo. (Picha zaidi ingia hapa)
No comments:
Post a Comment