Kikosi kazi cha watanzania wanaoishi Falme za UINGEREZA na EIRE YA KASKAZINI (TZUK Diaspora Taskforce, kwa kifupi, TZUK-DTF) kiliasisiwa na Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe mwaka 2014, kutokana na kutokuwepo na chombo/Jumuiya madhubuti ya kuwaunganisha Watanzania waishio hapa Uingereza
TZUK-DTF
ilianza na wajumbe 11 wakiwemo maofisa wa ubalozi 2 kikiwa na majukumu
makubwa ya kuwa kiunganishi kati ya watanzania na ubalozi wao hapa
Uingereza pamoja na kupanga na kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya
watanzania ambayo itakuwa shirikishi zaidi na endelevu. Mnamo mwishoni
mwa mwaka 2015, chini ya Naibu Balozi, Mheshimiwa Msafiri Marwa,
ilikubaliwa kwamba ili kutimiza malengo yake kwa ufanisi zaidi
yaliyohusisha kuratibu ufufuaji wa Jumuiya ya watanzania Uingereza na
kuhakikisha kwamba Jumuiya hiyo inakuwa na Katiba iliyo bora zaidi,
ilionekana ni vyema TZUK-DTF ikawa na wajumbe zaidi watakaojumuisha
watanzania wa kada mbalimbali walioko Uingereza wakiwemo waliokuwa
viongozi wa mikoa wa Jumuiya na baadhi ya wale walioshiriki katika
michakato ya uasisi wa katiba na uundwaji wa Jumuiya ya watanzania
Uingereza.
Kikosi
Kazi hiki kipya kilikutana rasmi tarehe 05 Mwezi wa Kumi na Mbili,
2015, chini ya uongozi na ulezi wa Mheshimiwa Naibu Balozi, Msafiri
Marwa, ambapo kiliainishiwa majukumu yake kama ifuatavyo:
1. Kujadili na kuziwekea mikakati ya ufumbuzi changamoto mbalimbali zilizokabiliwa na TZUK-DTF katika kutimiza majukumu yake ikiwemo na zile ambazo ziliikabili Jumuiya ya watanzania iliyokuwepo.
2. Kupitia
maoni ya watanzania yaliyokuwa yamekusanywa tayari, ikiwemo na katiba
za Jumuiya ili Jumuiya iwe na katiba bora zaidi itakayoongeza ufanisi
katika shughuli zaJumuiya.
3. Kuhakiki na kuboresha muundo wa Jumuiya utakaokidhi mahitaji ya sasa ya watanzania waishio Uingereza.
4. Kuzikusanya
na kuzipitia taarifa zote zitakazopatikana za fedha za Jumuiya enzi za
uhai wake na kuzijumuisha kwenye Jumuiya mpya itakayoundwa
5. Kutengeneza na kuratibu njia bora zamawasiliano miongoni mwa wanajumuiya.
6. Kusimamia
kipindi cha mpito kitakachopelekea kuundwa kwa Jumuiya ya watanzania
Uingereza ikiwemo kuratibu uanzishaji/uimarishaji wa Jumuiya za
watanzania za mikoani kwa mujibu wa katiba mpya, na
7. Kuandaa
na kusimamia mkutano mkuu wa watanzania wote wa Uingereza wenye
madhumuni ya kutoa ripoti nzima ya TZUK-DTF, kupitisha katiba mpya,
kutambulisha Kamati Kuu na uongozi mpya wa Jumuiya, kujadili na kuhakiki
mipango na mikakati ya shughuli mbalimbali za Jumuiya kwa mwaka ujao,
na Kikosi Kazi kuvunjwa rasmi na kukabidhi madaraka ya usimamiaji na
uendeshaji wa Jumuiya ya watanzania kwa uongozi mpya wa Jumuiya.
Kama watanzania wa Uingereza mlivyoshiriki katika upendekezaji wa katiba mpya na kutoa maoni juu ya Jumuiya yenu, tunaendelea kuwatia moyo kushiriki kwa moyo mmoja na wa kizalendo pindi tutakapoitisha mikutano ya watanzania kwenye mikoa mliyoko mwezekuhakikisha safari hii ya kuwa na Jumuiya iliyo/zilizo imara inafikia mwisho ulio mwema
Ahsanteni
No comments:
Post a Comment