Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akisalimiana na kumkaribisha
ofisini kwake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya,
Luana Reale (katikati) walipowasili jijini Mwanza kabla ya ziara ya
kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa
Ulaya.
MRATIBU
Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro
Rodriguez pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa
Ulaya, Luana Reale, wamesema wameridhishwa na miradi inayofadhili maeneo
kadhaa jijini Mwanza.
Wakizungumza
baada ya kutembelea Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Mwauwasa),
Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam
(DIT) na Radio ya Kijamii (Saut), walisema utekelezaji wa miradi hiyo
imewatia hamasa kubwa.
Awali
akizungumza katika ofisi za Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
(Mwauwasa), Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka hiyo, Anthony Sanga, alisema
mradi unaoendelea sasa wa kusambaza maji safi utakapokamilika utaweza
kuwafikia wakazi 54,000 badala ya 23,000 wa sasa.Sanga alisema mradi huo utakapokamilika Mei mwaka huu, utawafikia wakazi kwa asilimia 90 badala ya 68 za sasa.
“Mradi
ukishakamilika utafanikisha makusanyo ya Sh. Bilioni 1.4 kwa mwezi
badala ya kukusanya Sh. milioni 316 za sasa kwa mwezi, ukiwa na matanki
ya ujazo wa lita 33,400,” alisema Sanga.Akizungumzia
hilo, Rodriguez alisema baada ya kushuhudia miradi hiyo ukiwamo wa maji
taka chini ya ufadhili wa EU, amefurahishwa na hali ya miradi hiyo.
“Timu
yetu imetembelea Mwauwasa na kushuhudia miradi hiyo inayofadhiliwa na
Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya huduma ya maji kwa wananchi, pia tumeenda
kuangalia chanzo cha maji na yanapowekwa maji taka,” alisema Rodriguez.Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Prof. Kien Mteta,
alishukuru UN na EU kwa miradi hiyo na kuja kushuhudia ufadhili wao.
“Ufadhili
umelenga katika mambo matatu, moja kwenye maabara ambako vilinunuliwa
vifaa vya mbalimbali vikiwamo vya kutambua kansa, pili vifaa vya mionzi
kwa ajili kutambua vyanzo vya magonjwa,” alisema Prof. Mteta.Aidha,
alisema pia wafadhili hao walitembelea kitengo cha kutoa matibabu ya
mionzi ya kansa, ambacho kinawafunza baadhi ya watumishi wake na
upatikanaji wa mashine.
Mkuu
wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale
(katikati) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella mara
baada ya kuwasili ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Hospitali
ya Bungando yenye uwezo wa vitanda 950 iliyoanzishwa mwaka 1972 ni
miongoni mwa hospitali nne kubwa nchini ambazo hutoa tiba maalumu
ikihudumia watu milioni 16 katika mikoa minane ya kanda ya ziwa.Hospitali
hii inatoa tiba ya ugonjwa wa saratani kwa mifumo miwili. Moja kwa
kutumia onkolojia au patholojia na tiba kwa kutumia mionzi.
Toka
mwaka 2000 hospitali ya Bugando imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na
kampuni ya kitaliano ya TISSON ASSOCIATION ili kuboresha huduma zake
patholiojia na pia kuanza kutibu kansa mwaka 2009.
Wataliano
wamewezesha kufundishwa kwa wataalamu wa patholojia na onkolojia ya
tiba, vifaa tiba, dawa na kuwezesha ziara za za kifundi za watu wa
patholojia na utafiti.Uangalizi wa wagonjwa wa kansa na matibabu yao ulianza mwaka 2009 na kuelezwa kuwa kwa mwaka wagonjwa 3500 wa kansa huangaliwa.Huduma ya uangalizi ni pamoja na kufanya utambuzi, upasuaji na utoaji wa tiba ya kemo.
Mtaalamu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa
utambulisho wa ujumbe alioambatana nao kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella.Hata hivyo wagonjwa wanaohitaji huduma ya mionzi hukatiwa rufaa hospitali ya kansa ya Ocean (ORCI).
Kutokana
na kuzidiwa kwa hospitali ya Ocean Road katika tiba ya mionzi, serikali
iliamua kutanua huduma zake na kuzifikisha Bugando.Ili
kuwezesha haja ya serikali taasisi ya nguvu za atomiki duniani na ile
ya hapa nchini kupitia mpango wa ushirikiano wa kiufundi walianzisha
miradi kadha yenye lengo la kuwezesha huduma yenye tija kwa wagonjwa wa
kansa.Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanachangia
miradi hiyo imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha tiba ya
mionzi katika hospitali ya Bugando.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Idara ya
Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale katika ziara maalum ya
kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UN pamoja na EU jijini
humo.
Kutoka
kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza CP. Clodwig Mtweve, Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella pamoja na Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa
Ulaya, Luana Reale wakiwa wameshilikilia kuhamasisha utekelezaji wa
malengo mapya ya maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yamewafikia wakazi wa
jiji la Mwanza.
Mkuu
wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa Ulaya, Luana Reale
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi
wa Mazingira (Mwauwasa) mara baada ya kuwasili katika ofisi hizo jijini
Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony
Sanga, akitoa 'power point presentation' ya maendeleo ya mradi wa maji
unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya jijini Mwanza kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella, Mkuu wa Idara ya Siasa, Mawasiliano ya Umoja wa
Ulaya, Luana Reale aliyeambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony Sanga akitoa maelezo ya mradi kwa ugeni ulioambata na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Maji yakiwa kwenye hatua ya kutakatishwa ili yawe salama kwa watumiaji.
Mhandisi
wa ubora wa maji Mwauwasa, Godadi Mgwatu akitoa maelezo kwa mgeni ugeni
huo ulioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kukagua mradi
wa maji wa Mwauwasa jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa), Mhandisi Anthony
Sanga akitoa maelezo kwa ugeni huo ya namna ya maji yanavyochujwa na
kusafisha kwa kutumia mtambo maalum uliopo mbele yao. (Picha zaidi za ziara hii Bofya hapa)
No comments:
Post a Comment