Mkurugenzi Mkuu wa Britam Tanzania Bw. Stephen Lokonyo (kulia)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Biashara ya Bima Britam group Bw.
Steven Wandera muda mfupi baada ya mkutano na waandishi wa habari
katika uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni hiyo ya Bima hapa nchini,
uzinduzi uliofanyika juzi Hyatt Regency hotel jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Biashara za Kimataifa Britam group Bw. Kennedy Aosa (kulia)
akibadilishana mawazo na Meneja Mauzo wa Britam Tanzania, Bw. Godfrey
Mzee (kushoto) na Afisa Mkuu Uendeshaji Britam Tanzania Bw. Sodson
Manatsa (katikati) muda mfupi mara baada ya kumaliza mkutano na
waandishi wa habari katika uzinduzi rasmi wa shughuli za kampuni hiyo
hapa nchini. Uzinduzi huo uliofanyika juzi Hyatt Regency hotel jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Biashara ya Bima Britam group Bw. Steven Wandera (wa kwanza kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi
rasmi wa shughuli za kampuni ya Bima ya Britam Tanzania nchini. Uzinduzi
wa kampuni hiyo ulifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam juzi. (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Tanzania Bw.
Stephen Lokonyo.
Meneja
Mauzo wa Britam Tanzania, Bw. Godfrey Mzee (kushoto) akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa
shughuli za kampuni ya Britam Tanzania hapa nchini ikiwa ni moja ya
juhudi zinazofanywa na Britam group kujipanua kikanda.Mkutano huo
ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
(Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Tanzania Bw. Stephen Lokonyo .
Mkurugenzi
wa Biashara za Kimataifa Britam Group Bw. Kennedy Aosa (katikati)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa
Kampuni ya Britam Tanzania hapa ncnini ambayo inayojishughulisha na
masuala ya bima. Katika upanuzi wa soko lake Britam Group imeingia rasmi
katika soko la Tanzania ambapo uzinduzi ulifanyika juzi katika hoteli
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo aliwahakikishia
watanzania kuwa lengo la Britam ni kuhakikisha kuwa inabadilisha
biashara ya bima hapa nchini na kuwa chaguo la watanzania.
Mgeni
rasmi Jaji (mstaafu) Joseph Sinde Warioba akipeana mkono na Mkurugenzi
Mtendaji wa Britam Group Dk. Benson Wairegi muda mfupi baada ya
mheshimiwa huyo kuzindua rasmi Kampuni ya Britam Tanzania
inayojishughulisha na masuala ya bima katika soko la Tanzania, uzinduzi
huo ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Jaji (mstaafu) Joseph Sinde Warioba (katikati) akibadilishana
mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Group Dk. Benson Wairegi (kulia)
na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania Bw. Steven
Lukonyo (kushoto) muda mfupi baada ya mheshimiwa huyo kuzindua rasmi
Kampuni ya Britam Tanzania inayojishughulisha na masuala ya bima katika
soko la Tanzania, uzinduzi huo ulifanyika juzi katika hoteli ya Hyatt
Regency jijini Dar es Salaam.
SHIRKA
la Britam Holdings linaloongoza katika huduma za kifedha limefanikiwa
kuzindua huduma zake nchini Tanzania baada ya kukamilisha mchakato wa
kuunganisha kampuni ya Real Insurance pamoja na shirika la Britam
lililopo nchini Kenya.
Uzinduzi
rasmi wa shirika la bima la Britam Tanzania ni moja wapo ya mkakati wa
shirika mama la Britam kukuza biashara yake ya bima na kuimarisha uwepo
wake katika kanda za kusini na Mashariki mwa Afrika wakilenga makundi ya
watu wasio na bima.
Takwimu
za hivi karibuni zinaonyesha usajili wa bima Tanzania ni chini ya
asilimia moja la pato la taifa, kiashirio cha chini sana ukilinganisha
na mataifa yaliyoendelea pamoja na mataifa mengine ya Afrika. Britam
inatazamia kupunguza pengo hilo kwa kuleta huduma za bima za kipekee
zenye ufumbuzi wa mahitaji ya watanzania.
Britam
ni shirika lenye kutoa huduma mbalimbali za kifedha na limesajiliwa
nkwenye soko la hisa mjini Nairobi. Shirika lina maslahi kanda nzima ya
masharika na kusini mwa Afrika, likitoa huduma zake nchini Kenya,
Uganda, Sudan ya Kusini, Mozambique na Malawi. Shirika linatoa huduma
mbali mbali za kifedha zikiwemo bima, benki pamoja utunzaji mali.
Akiongea
jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Britam Dk.
Benson Wairegi alisema kampuni hiyo itatumia uzoefu wake wa miaka 50
katika masuala ya kifedha, jina lake lina nguvu na kuaminika ndani ya
nchi saba barani Afrika, nguvu kazi kubwa ya waajiriwa wake pamoja na
mfumo wake thabiti wa teknolojia.
“Uzinduzi
wa Britam nchini Tanzania ni kiashirio cha hatua muhimu iliyopigwa na
shirika katika mkakati wake wa kukuza bidhaa na huduma za bima katika
soko. Ndani ya Britam kuna huduma na bidhaa nyingi za kifedha katika
masuala ya bima, usimamizi wa mali pamoja na benki. Wateja wetu nchini
wataweza kupata huduma hizo zote chini ya paa moja” alisema Dk. Wairegi.
Dk.
Wairegi alidokeza pia jinsi Britam ni chapa inayoheshimika sana nchini
Kenya, likiwa linaendesha shughuli zake kwa miaka zaidi ya 40, shirika
limekuwa mstari wa mbele katika huduma wanazotoa.
Bw.
Stephen Lukonyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Insurance Tanzania
alisema kampuni tayari ina matawi saba nchini, Dar es Salaam, Arusha,
Mwanza, Dodoma, Mbeya, na Mtwara, huku matawi zaidi yakiwa mbioni
kufunguliwa katika siku zijazo.
“Matawi
haya yatahudumia maeneo ambayo huduma za bima bado hazijafika vya
kutosha. Wananchi sasa wataweza kupata huduma zote kwa urahisi na
unafuu” alisema Lokonyo.
Bw.
Lukonyo aliongezea kwa kusema tayari kampuni wamepokelewa vizuri sana na
mawakala pamoja na washika dau katika sekta ya bima Tanzania, huku
akiomba kuendelea kuungwa mkono ili kuwezesha kampuni yake kutoa huduma
bora kwa wateja na hivyo kusaidia kukuza soko la bima nchini.
Alisema
kampuni imepiga hatua kuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi wa bidhaa na
hivi karibuni watazindua bima ya afya na usafiri katika soko la
Tanzania. Kampuni pia inatazamia sekta ya mafuta na gesi pamoja na sekta
ya kilimo.
No comments:
Post a Comment