Hivi
juzi tumeshuhudia ufunguzi wa daraja la Kigamboni ambalo Mh. Rais Dr.
John Pombe Mgufuli alilipa jina la daraja la Nyerere. Daraja hili ni
matunda ya uwekezaji wenye tija unaofanywa na Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii la NSSF.
Shirika
hilo kwa kushirikiana na serikali limeweza kujenga daraja lenye urefu
wa mita 680 likiwa na barabara sita; tatu zikielekea Kigamboni na tatu
zikitokea Kigamboni. Daraja hili lina njia ya watembea kwa miguu yenye
upana wa mita 2.5 kila upande.
Daraja
hilo limejengwa kisasa na kampuni ya China Railway Construction
Engineering Group iliyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya
China Railway Major Bridge Group kutoka nchini China.
Kukamilika
kwa ujenzi wa daraja hili, kumejumuisha barabara za kufika katika
daraja hili zenye jumla ya urefu wa kilomita 2.5. Katika ujenzi wa
daraja hili, Shirika la NSSF limetoa asilimia 60 ya gharama za Ujenzi na
Serikali asilimia 40 ya gharama hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliotembela daraja hilo hivi karibuni, Meneja
wa Mradi huo kutoka NSSF, Muhandisi Karim Mattaka alisema daraja la
Kigamboni limejengwa ili kuondoa kero ya siku nyingi ya usafiri kwa
wakazi wa Kigamboni na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla, kuimarisha
hali ya uchumi wa Mkoa huu wa Dar es Salaam, mikoa ya jirani na nchi kwa
ujumla pamoja na kuimarisha hali ya uchumi wa shirika, kuliwezesha
shirika kuboresha na kulipa mafao kwa kutunza thamani ya fedha kupitia
kitega uchumi hiki.
Faida
zitokanazo na uwekezaji huo kwa mujibu wa Muhandisi Mattaka ni faida ya
moja kwa moja kwa wanachama kwani huingizwa katika akaunti zao pindi
wanapochukua mafao yao pamoja na kulipia matibabu yatolewayo bure kwa
wanachama.
“Daraja
hili linadhihirisha uwezo wa shirika katika nyanja za uwekezaje na
kuwapa wanachama uhakika kuwa pesa zao ziko salama,’’.
“Ni
dhahiri kuwa daraja litaondoa usumbufu mkubwa ambao wananchi walikuwa
wanaupata na hata wakati mwingine kupoteza maisha, kwani vivuko vya
Kigamboni vikiwa vimeharibika wananchi walikuwa wanatumia mitumbwi
ambayo wakati mwingine sio salama,.’’ Alisema
>
Kukamilika kwa daraja hilo kunaelezwa kuwa kutachangia sana katika
kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Kigamboni,
Jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Inaelezwa
kuwa daraja hilo sasa limefungua fursa kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kukamilisha utaratibu wa kujenga mji wa kisasa
(Kigamboni Elite City) utakaokuwa na nyumba za kisasa, kuongeza
ufanisi katika utalii kwa kujenga mahoteli ya kitalii katika fukwe
zilizopo eneo la Kigamboni, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoa ya
kusini mwa nchi yetu na hata nchi jirani zetu, kupanua kilimo cha
matunda, mboga na mazao mengineyo yanayozalishwa katika eneo hili.
“Wakulima sasa wataweza kufikisha bidhaa zao sokoni kwa urahisi zaidi na hivyo kuongeza kipato chao,’’ aliongeza.
Kwa mujibu wa Muhandisi Mattaka daraja hilo vilevile litarahisisha uwezekano wa upanuzi wa bandari upande wa Kigamboni.
“Kwa
ujumla Daraja la Kigamboni litaboresha sana usafiri ndani ya Mkoa wa
Dar es Salaam na kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa magari
unaolikabili Jiji la Dar es Salaam hasa baada ya ujenzi wa barabara ya
Dar es Salaam – Chalinze kwa kiwango cha “Expressway” ambayo
itaunganishwa na Bandari ya Dar es Salaam kupitia Daraja la
Kigamboni.,’’ alisema
Muhandisi
Mattaka alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wa shirika hilo kuhusu
usalama wa fedha zao na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa kiwango
cha kimataifa.
Kwa
upande Muhandisi wa Mradi huo kutoka kampuni ya China Railway
Construction Engineering Group iliyotekeleza mradi huo kwa kushirikiana
na kampuni ya China Railway Major Bridge Group kutoka nchini China,
Muhandisi Jamal Mruma alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu watumiaji wa
daraja hilo kwa kuwa limetengenezwa katika ubora na teknolojia ya hali
juu kabisa.
“Ni
aina ya mradi bora kabisa kuwezeshwa na NSSF pamoja serikali na
hatimaye kutekelezwa kampuni bora katika masuala ya ujenzi kutoka
China.Niwatoe hofu watumiaji wa daraja pamoja na wanachama wa NSSF kuwa
wajivunie mradi huu unafaida kubwa sana kwao na taifa kwa
ujumla...waulinde na wajivunie haya ni matunda ya pesa zao,’’ alisema.
Akizungumza
katika hafla ya ufunguzi wa daraja, Naibu waziri wa kazi, ajira, vijana
na walemavu aliwaasa waajiri wasiopeleka michango yao katika mifuko ya
hifadhi ya jamii kutekeleza sheria kwa kuchangia kwa wakati ili kuepuka
usumbufu wakati wanachama watakapokua wanahitaji mafao yao.
No comments:
Post a Comment