Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili katika kata ya Hembeti, Kijiji cha Dihinda kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima nawafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.
Katika
Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016
kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji
ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.
Wakati
huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza
kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si
vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali
imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika
sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu
zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya
kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo
kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la
mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara
yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda
uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na mama
mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake kukatwa katwa mapanga na watu
wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji cha Dihinda.Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero.Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya ya
Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara yaliyosababishwa na uhusiano
mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la kata ya Hembeti.Waziri
wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya
Mvomero, Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa wakati
wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya wakulima
nawafugaji wilayani mvomero.
Picha na Sanga Festo Jr.
No comments:
Post a Comment