WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaonya watendaji wa halmashauri nchini kwamba
atakayebainika ametumia vibaya fedha za Serikali atang'olewa kazini kwa
sababu Serikali ya Awamu ya Tano haina mchezo na mtu.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Desemba 20, 2015) wakati akizungumza
na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo Lindi mjini.
"Natoa
onyo kwa watendaji wote wa halmashauri. Fedha ya Serikali itakayotumwa
kwenu halafu mtu aifanyie ubadhirifu, ole wake. Yeyote atakayebainika
kuzitumia kwa ubadhirifu fedha hizi tutamng'oa. Wako wasomi wengi huko
nje tena wazuri tu, wanasubiri kupata ajira."
"Nataka
watumishi wa umma watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano
inajielekeza kujali wananchi. Wao wana dhamana ya kuwasilikiliza na
kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha wanatatua kero zinazowakabili, "
alisema huku akishangiliwa na wengine wakisema huyu sasa ni Sokoine wa
pili. (Edward Moringe Sokoine alikuwa ni Waziri Mkuu katika Serikali ya
Awamu ya Kwanza).
Waziri
Mkuu ambaye amewasili Lindi leo, aliwaeleza wakazi hao kwamba amekuja
kuwashukuru wazee na wana Lindi kwa dua zao na kuwaahidi kwamba
hatawaangusha Rais John Pombe Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu
Hassan kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuwatumikia Watanzania katika
ngazi ya Uwaziri Mkuu.
Waziri
Mkuu pia alimpa kazi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Jordan Rugimbana ya
kuhakikisha anaufufua uwanja huo na kuurudisha kwenye enzi yake
ulivyokuwa maarufu katika mikoa yote ya Kusini. "Uwanja huu lazima
uboreshwe kwa sababu unanikumbusha mwaka 1984 wakati nachezea timu ya
Amri Rangers. Kulikuwa na ukoka wa nguvu hapa uwanjani. Kwa hiyo timu
aliyoiunda Mkuu wa Mkoa itafanya kazi lakini pia iwajumuishe Meya na
mbunge wa Lindi Mjini kwa sababu huu uwanja ni mali ya Halmashauri ya
Lindi, " alisema.
Akielezea
kuhusu mipango ya Serikali kuendeleza sekta ya viwanda, Waziri Mkuu
alisema hivi karibuni mkoa huo utapata wawekezaji kwenye sekta ya gesi
baada ya kampuni ya BG kutoka Uingereza kupata umiliki wa eneo la
Kikwetu ili wajenge mitambo ya kusafisha gesi.
Aliwataka
wananchi wa mkoa huo wawekeze kwenye ujenzi wa hoteli na nyumba za
kulala wageni ili ifikapo Agosti mwakani, watu wanaokuja kushiriki
maonyesho ya NaneNane kitaifa mkoani humo wasipate taabu ya malazi kama
ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zawadi ya shati la asili la Wamwera
na Mzee Saidi Issa Hanga katika mkutano wa hadhara aliouhutubia mjini
Ruangwa Desemba 20, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary wakisalimiana na wazee wa Ruangwa
kabla ya mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu mjini Ruangwa
Desemba 20, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia silaha za asili alizokabidhiwa na
wazee wa Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini hapo
Desemba 20, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa alipokea zawadi ya rungu kutoka kwa Mzee Issa
Juma Nangalapa ikiwa ni ishashara ya kumtaka awaadhibu wotw wanaokiuka
sheria. Alikuwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia mjini Ruangwa
Desemba 20, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia moja kati ya zana na silaha za asili
alizokabidhiwa na wazee wa Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara
mjini hapo Desemba 20, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Lindi akiwa njiani kwenda kijijini kwake Nandagala
wilayani Ruangwa, Desemba 20, 2015.Katikati ni Waziri wa habari,
Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Nauye.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wapigakura wake baada ya kuwasili
kijijini kwake Nndagala wilayani Ruangwa kwa mapumziko mafupi Desemba
20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment