Na Vero Ignatus , Wazalendo 25 Blog -Arusha
Hatimae kampeni ya abiria paza sauti imefungwa rasmi jijini Arusha na mkuu wa mkoa wa Arusha mh,Filex Ntibenda katika stendi kuu ya mabasi na kuhudhuriwa wa viongozi mbali wa Jeshi la polisi akiwemo kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Naibu kamishna wa polisi Liberatus Sabas, Kamanda wa usalama barabarani Mkoa Arusha Marson Mwakyoma,Mkuu wa kituo usalama barabarani Emiliani Kamuhanda ,Sumatra,,viongozi wa usafirishaji ,madereva na abiria.
Ntibenda amesema kuwa abiria wengi wamekuwa wakipoteza maisha wanapokuwa safarini,amewataka abiria kuwa timamu watoe taarifa kwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani pale wanaoona dereva anapokuwa na mwendo kasi akiwa barabarani, amelewa,akizungumza na simu,au kuovateki pasipostahili .
Sambamba na hayo mkuu wa mkoa amewasema kuanzia januari mosi kila mwenye silaha ya moto jijini Arusha aisalimishe polisi na aanze hatua ya kujiandikisha upya,na amesema wengi watanyanganywa silaha hii ni kutokana na matumizi mabaya ya silaha haswa kwa jiji la ARUSHA.
Naye kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema kuwa matukio yanayoongoza kwa kusababisha vifo vingi ni ajali za barabarani,ambapo ajali moja inaweza kusababisaha vifo vya watu 30 hadi 50 amesema usimamiaji wa sheria za usalama barabarani ni jambo lisilo epukika na amesema askari wa usalama barabarani, wakiwa legelege ni kwamba wameruhusu watu kufa bila sababu .
Kamanda Sabasi ameongeza kuwa sheria lazima isimamiwe ili kudhibiti makosa yanayojitokeza barabarani,ili Watanzania wasiendelee kupoteza maisha bila ya sababu,na amewashukuru Mabalozi wa usalama barabarani Arusha ( RSA)kwa kutoa elimu kwa abiria,kufahamu haki zao kupaza sauti ns siyo kukaa kimya.
Kamanda amewaonya abiria waache uchochezi wa uvunjifu wa sheria kwa kuwasifu madereva ambao hawafuati sheria, lakini tatizo linapotokea kama ajali wao ndio wakwanza kulalamika na kuwalaumu wale ambao wanafuata sheria za usalama barabarani aidha amesema kuwa kila mmoja atimize wajibu wake dereva afuate sheria zote za usalama barabarani na abiria awe mdau mkuu wa kupunguza ajali zinazoepukika.
No comments:
Post a Comment