Usaili huu utajumuisha warembo mbalimbali ambao wana vigezo vya kushiriki na hatimaye kuingia katika kambi ya Miss Universe Tanzania itakayofanyika hivi karibuni.
Dar es salaam inakuwa mkoa wa mwisho baada ya mikoa mbalimbali kutuma warembo waliojitokeza kuchukua fomu katika kuwania uwakilishi wa taji la Miss Universe Tanzania2015. Mikoa iliyoshiriki kutuma wawakilisi mwaka huu ni Arusha, Tanga, Mbeya, Iringa na Mwanza.
Warembo wote wenye sifa wanaombwa wajitokeze hata kama bado hawajachukua fomu kwani ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss Universe Tanzania pia washindi wa pili na wa tatu hupata fursa ya kushiriki katika mashindano mengine madogo ikiwemo Miss Earth kwenda kushindana kimataifa kama wenzao waliotangulia.
No comments:
Post a Comment