Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania,
Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana
saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa EU, Eric Beaume. (Picha na Francis Dande)
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya
(EU), nchini Tanzania,
Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana
saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya
(EU), nchini Tanzania,
Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akisaini hati na Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana
saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza katika hafla ya kutiliana
saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA
ya Ulaya (EU)imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini
yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN), ruzuku Euro 200,000 sawa na sh.
Milioni 478.
Utilianaji
saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini , Alvaro Rodriguez na
Balozi wa EU, Filiberto Sebregondi.
Sebregondi
alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza mfano wa namna bora Mashirika ya UN
yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi moja katika kuboresha maisha ya watu.
Naye
Rodriguez, alisema fedha hizo zimelenga kusaidia miradi ya pamoja ya EU NA UN
ya mawasiliano, uragibishi, uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.
Rodriguez,
alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania wakati
nchi inajipanga kutekeleza malengo ya endelevu SDGs.
“Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati sisi UN na
washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo na mtanzania
atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,” alisema.
No comments:
Post a Comment