Naibu Mwenyekiti Ofisi Kuu ya Hijja Tanzania (BIITHA), Yusuf Musun (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kusogezwa mbele muda wa kujisajili kwenda Hijja kutoka Juni 15 hadi Agosti 25 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Habari wa Biitha, Hamisi Tembo na Mratibu wa Biitha, Abdallah Khalid.
Mkutano na wanahabari ukiendelea. | Na Dotto Mwaibale MAHUJAJI nchini wametakiwa kujitokeza kujisajili katika taasisi zilizosajiliwa kisheria ili kujiandaa kwenda katika ibada ya hija itakayofanyika nchini Saud Arabia Septemba 16 mwaka huu. | Kauli hiyo imetolewa Dar es Salaam leo na Naibu Mwenyekiti wa Ofisi Kuu ya Hijja Tanzania Bara na Zanzibar, Yusuf Musun wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusogeza muda huo kutoka Juni 15 hadi Agosti 25 mwaka huu, Alisema kusogeza mbele kwa muda wa usajili ni kutoa fursa kwa wanaotarajia kwenda kuhiji ili waendelee kujitokeza kwa wingi kujisajili katika taasisi zilizo rasmi. | Alisema wananchi wenye nia ya kwenda hijja lakini hawana fedha za kulipa kwa mkupuo wanaweza kwenda kulipia kidogo kidogo kwenye ofisi husika. | Musun alisema lengo la kutoa mwito huo ni kuhimiza watu wanaolipa fedha zao binafsi na wale wanaolipiwa na mashirika mbalimbali kujisajili kwa wakati ili usajili uweze kumalizika katika muda uliopangwa. | "Waislamu wengi hawatoe hela zao kutoka mfukoni wengi wao wanaolipiwa na mashirika mbalimbali hivyo tunawahimiza wajisajili kwa wakati kwa ajili ya safari hiyo ya hijja.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062) | |||||||||
No comments:
Post a Comment