Teknolojia Yetu :TCRA Yawahimiza Wananchi Kutumia kwa Usahihi Mawasiliano - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 7 August 2015

Teknolojia Yetu :TCRA Yawahimiza Wananchi Kutumia kwa Usahihi Mawasiliano


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) Kanda ya Kaskazini,Annette Mahimbo Matindi.

Wananchi wanaofika kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji(Taso)Nane nane Njiro jijini Arusha wametakiwa kufika kwenye banda la TCRA kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na Mamlaka hiyo muhimu kwa wananchi na uchumi kwa ujumla.


Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) Kanda ya Kaskazini,Annette Mahimbo Matindi amesema kuna umuhimu mkubwa wananchi kufahamu utendaji kazi wa taasisi hiyo badala ya kuilalamikia bila kujua mipaka na wajibu wake.

Amesema wakulima na wafugaji ili kunufaika katika shughuli zao hawana budi kutumia kwa usahihi  huduma za mawasilino ili kukuza biashara zao.

"Nitumie fursa hii kuwataka wananchi wote kutumia kwa usahihi huduma za mawasiliano badala ya matumizi yasiyofaa na ambayo wakati mwingine watajikuta kwenye mikono ya vyombo vya dola,"amesema Annette

Amesema wakulima na wafugaji ni sehemu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania hivyo  mawasiliano ni nyenzo muhimu kwao. 

No comments:

Post a Comment