Kulia ni Kamanda Mpinga akiwa na mabalozi
wa RSA wakikabidhi vifaa hivyo kwa maofisa wa Kitengo cha Taarifa cha
Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi.
<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>
Na Augustus Fungo, Admin 1 RSA
<<<<<<<<<<>>>>>>>>>>>>>
Na Augustus Fungo, Admin 1 RSA
Hivi karibuni imejitokeza njia mpya ya kusaidia kupambana
na wimbi la ajali za barabarani, ambapo pamoja na faini madereva
wanaokiuka sheria za barabarani wamekuwa wakipigwa picha na baadaye
picha hizo kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii au magazetini na hata
wakati mwingine kwenye televisheni. Mathalani katika mtandao wa facebook
kundi la Mabalozi wa Usalama Barabarani maarufu RSA wakishirikiana na
polisi hutumia mbinu hii kuwapiga picha wakiukaji wa sheria za
barabarani kisha kuzituma katika kituo cha mawasiliano cha polisi
maarufu TCC.
Kituo hiki huwatumia picha hizi ambazo pia ni ushahidi
askari waliopo barabarani, ili kuwezesha askari hawa kukamata magari
husika. Baada ya kukamata magari husika askari aliyehusika kukamata
humwandikia faini mkosaji, kumpiga picha na kuituma kwenye kituo cha
mawasiliano ya polisi(TCC) ambacho na chenyewe hutoa mrejesho kwa watoa
taarifa. Picha hizo hatimaye kuwekwa kwenye mtadao wa facebook, hutumika
kuandaa vipindi vya televisheni mfano, ni kipindi cha ‘Aibu
yako”kinachorushwa na televisheni ya ITV na pia picha hizo huhifadhiwa
na kikosi cha usalama barabarani kwaajili ya kumbukumbu na kama rejea
iwapo dereva husika atalirudia kosa hilo.
Njia hii mpya ambayo inaitwa kutaja na kuaibisha, ama kwa
kiingereza “Naming and Shaming”ni mbinu maarufu sana inayotumika sit u
nan chi nyingi za ulaya bali pia hata mashirika ya haki za binadamu kama
Human Rights Watch, hutumia mbinu hii kuyaaibisha mataifa yaliyokubuhu
kwa ukiukaji wa haki za binadamu. Saudi Arabia kupitia sheria yake ya
makosa ya mtandao (Anti-cyber-crime law (Royal Decree No. M/17 dated 8
Rabi1 1428) imepitisha mbinu hii kama mojawapo ya adhabu. Mbinu kama hii
hutumika pia katika nchi nyingi za ulaya kuwaaibisha watu au makampuni
yanayokwepa kodi. Moja ya makampuni yaliyowahi kuathirika na kadhia hii
ni kampuni ya kahawa ya Starbuck. Januari 15, 2015, serikali ya
Uingereza iliwataja na kuwadhalilisha waajiri 37 wa Uingereza
walioshindwa kulipa kima cha chini kwa wafanyakazi wao. Mwandishi James
Meernick(2012), anaitaja njia hii kama chaguo kuu la mashirika mengi ya
kimataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa.
Njia hii hutumika ikiaminika kwamba kumuweka mtu au taasisi
hadharani ili aweze kujiona mwenyewe, aonwe na familia yake, marafiki
zake, na hata waajiri wakati akitenda kosa inasaidia kumfanya mtu
ajitafakari na kutorudia kosa au pia kuwafanya wanaomzunguka kumpa
shinikizo la kufuata sheria au kuheshimu haki za wengine. Baadhi ya
wadau hapa nchini wameipokea mbinu hii kwa hisia tofauti. Wengine
wamedai kwamba ni kinyume cha sheria japokuwa hawajaweka kutaja ni
sheria gani hasa inayokiukwa kwa kufanya hivyo; wengine wamedai ni
kuingilia usiri(privacy) yam tu bila kusema ni kwa vipi siri yam tu
inaingiliwa pale anapotenda kosa. Wameshindwa kuushawishi umma kuelewa
je, mtu anapokuwa mathalani anatanua barabarani, au anaovateki
pasiporuhusiwa au anakimbia kwa speed zaidi ya 80 akakamatwa akapigwa
picha ni kwa jinsi gani anadhalilishwa zaidi ya kuaibishwa? Maana wakati
anapigwa hiyo picha kwanza anakuwa ameshakubali kosa; pili, anakuwa
hajavuliwa nguo wala kurushwa kichurachura, kupigwa au kufungwa pingu.
Isitoshe wapinzani wa mbinu hii wameshindwa kuwashawishi
watanzania kuelewa iwapo kumpiga picha mkosaji barabarani ni kosa,
inakuwaje au ni mara ngapi watuhumiwa wamekuwa wakipigwa picha
wanapofikishwa mahakamani? Je, ni mara ngapi kumekuwa na matukio mfano
ya ujambazi na watuhumiwa wa ujambazi katika eneo la tukio au
walipokamatwa vyombo vya habari vimekuwa vikiwapiga picha. Je, huku si
kuvunja sheria? Itakumbukwa ITV wamewahi kurusha kipindi maalumu
kinachoonesha askari wakipokea rushwa,mbona hili halikusemewa? Ni mara
ngapi polisi wamekuwa wakitoa picha wa watu wanaotafutwa kwa uhalifu
(wanted), ni mara ngapi waajiri wamekuwa wakitoa picha za wafanyakazi
wao waliofukuzwa kazi kwa makosa ya kutokuwa waaminifu? Iweje leo picha
za wakosaji wa barabarani tu ionekane kuwadhalilisha?
Hoja ya kwamba dereva huyu ana maisha yake mengine
ambayo yanaathiriki kutokana na kupigwa picha, haina mashiko kwakuwa lengo la mbinu ya kutaja na kuaibisha ni kumfanya muhusika aone aibu kwa upuuzi alioufanya na kuweza kujirekebisha. Dereva anayejua kuwa hiyo inaweza kumuharibia hadhi yake huko baadae atakuwa makini zaidi kutokiuka sheria za barabarani au kuchezea maisha ya watanzania wasio na hakia. Gari za serikali, mashirika ya umma, miradi, nk haziko juu ya sheria. Bila kujali operesheni wanayofanya au lengo la safari yao hawapaswi kuvunja sheria, na endapo watakuwa wamevunja sheria kwa sababu ya kwenda kuhudhuria dharula husika, askari aliyesimamisha hilo gari akiridhika na sababu hiyo hataaandika faini wala kupiga picha, kwa hiyo hakuna kitakachoathirika. Na endapo kuna hofu ya matumizi mabaya ya hizo picha, atakayewajibika ni huyo anayetumia vibaya picha hiyo ili mradi tu picha halisi(original) ya tukio zima ipo na ndiyo itakayotumika kama ushahidi dhidi yam tu aliyeitumia picha hiyo vinginevyo.
ambayo yanaathiriki kutokana na kupigwa picha, haina mashiko kwakuwa lengo la mbinu ya kutaja na kuaibisha ni kumfanya muhusika aone aibu kwa upuuzi alioufanya na kuweza kujirekebisha. Dereva anayejua kuwa hiyo inaweza kumuharibia hadhi yake huko baadae atakuwa makini zaidi kutokiuka sheria za barabarani au kuchezea maisha ya watanzania wasio na hakia. Gari za serikali, mashirika ya umma, miradi, nk haziko juu ya sheria. Bila kujali operesheni wanayofanya au lengo la safari yao hawapaswi kuvunja sheria, na endapo watakuwa wamevunja sheria kwa sababu ya kwenda kuhudhuria dharula husika, askari aliyesimamisha hilo gari akiridhika na sababu hiyo hataaandika faini wala kupiga picha, kwa hiyo hakuna kitakachoathirika. Na endapo kuna hofu ya matumizi mabaya ya hizo picha, atakayewajibika ni huyo anayetumia vibaya picha hiyo ili mradi tu picha halisi(original) ya tukio zima ipo na ndiyo itakayotumika kama ushahidi dhidi yam tu aliyeitumia picha hiyo vinginevyo.
Ni ushauri wetu kuwa askari waendelee na mbinu hii ili
wavunja sheria waaibike na kuweza kujirekebisha. Haiwezekani dereva
amesomea amejaribiwa na kupewa leseni, anajua amebeba abiria kwenye gari
lake halafu aendeshe kwa mwendo hatarishi, ayapite magari mengine kana
kwamba amebeba viazi, au abiria ni mateka wake. Faini peke yake
hazisaidii. Tungependa hata siku moja mahakama imhukumu mkosaji kufagia
barabara za kariakoo kwa wiki zima badala ya kumpeleka jela hii
ingesaidia zaidi kurekebisha watu. Kama taifa lazima tuwe na adhabu
mbadala.
Na kwakuwa hakuna sheria inayovunjwa kwam tu kupigwa picha
wakati akitenda kosa na kuwekwa hadharani, mbinu hii bado itaendelea
kuwa sahihi ili wahusika waache kutenda makosa ambayo yanagharimu si tu
maisha ya watanzania bali pamoja na uchumi wa nchi. Jeshi la polisi ni
jeshi lenye ueledi na wataalamu mbalimbali hivyo litaendelea kubuni
mbinu mbalimbali za kurekebisha tabia na kutekeleza sheria.Hii ndio
imani yangu kwa taasisi hii muhimu nchini Tanzania, wananchi
tushirikiane nao.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu sote.
No comments:
Post a Comment