Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Idadi ya Watu (UNFPA) Tanzania, wameandaa warsha ya kuhamasisha na
kujenga uwezo kwa watumishi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa
kuhusu kujumuisha masuala ya vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Warsha
hiyo inafanyika katika vituo vya Mwanza na Musoma. Katika kituo cha
Mwanza warsha inafanyika tarehe 8 na 9 Juni 2015, kituo ambacho
kinajumuisha Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za mikoa ya Mwanza,
Shinyanga na Geita.
Washiriki
wa warsha hii ni Makatibu Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu),
Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya
Msingi wa Wilaya na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya.
Mgeni
Rasmi Bw. Ibrahim D. Kalengo, Mtakwimu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango ambae anamwakilisha Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, akitoa neno la ufunguzi kwa ajili ya warsha hiyo kuanza rasmi.
Afisa
kutoka UNFPA anaeshughulika na vijana Bi. Tausi Hassan, akiwashukuru
washiriki kwa kuitikia wito na kushiriki kikamilifu warsha hiyo.
Bw.
Ramadhani Hangwa afisa kutoka UNFPA anaeshughulika na Program ya Idadi
ya Watu na Maendeleo, akitoa neno kwa washiriki kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi ili afungue semina hiyo.
Mwezeshaji
Dr. Deograsias P. Mushi ambae pia ni Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam na Mtafiti wa Ecom Research Group akishusha nondo kwa
wanawarsha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu ujumuishaji wa masuala ya
vijana katika mipango ya Mkoa na wilaya.
Washiriki
wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu
Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa
Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa
Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi wakati
wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika katika Hotel ya
Gold Crest jijini Mwanza.
Washiriki
wa warsha kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita ambao ni Makatibu
Tawala Wasaidizi (Mipango na Uratibu), Maafisa Watakwimu (RS), Maafisa
Mipango wa Wilaya, Maafisa Elimu ya Msingi wa Wilaya na Maafisa
Maendeleo ya Jamii wa Wilaya wakimsiliza kwa makini mwezeshaji.
No comments:
Post a Comment