Michezo : Mhe. Pinda Afungua Mashindano ya UMISETA, Jijini Mwanza - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 11 June 2015

Michezo : Mhe. Pinda Afungua Mashindano ya UMISETA, Jijini Mwanza


Msanii wa ngoma ya Kisukuma akicheza na nyoka aina ya chatu wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza amabko Juni 10, 2015 alifungua michezo ya UMISETA.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya UMISETA wakipita kwa mandamano mbele ya mgeni rasmi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika ufunguzi wa mashindano hayo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akikagua kundi la waamuzi na walimu wa michezo wa shule za sekondari baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya kanda ya ziwa baada ya kufungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 10, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga mpira wakati alipofungua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Juni 10, 2015.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda akirusha mpira wa kikapu wakati alipozindua mashindano ya UMISETA kwenye uwanja wa CCM Kirumba Juni 10, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment