Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (katikati) akionyesha kabrasha lenye fomu ya kuomba
kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa
(Nec) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu. Kulia
ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la
uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini
Dodoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akisaini kitabu kabla ya kuchukua fomu ya kuomba
kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya
katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini, Dodoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akiwaonyesha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kabrasha lenye fomu ya kuomba
kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM
kabla ya kuanza kuzungumza na kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa
habari. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio
hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba
kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
Waziri Chikawe ambaye alijibu maswali ya waandishi wa habari kiufasaha
huku akishangiliwa na wanachama hao, alisema yeye ni kiongozi mwenye
uzoefu mkubwa na pia akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo
ataendeleza mapambana zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga,
maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa
maendeleo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba
kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,
Waziri Chikawe ambaye alijibu maswali ya waandishi wa habari kiufasaha
huku akishangiliwa na wanachama hao, alisema yeye ni kiongozi mwenye
uzoefu mkubwa na pia akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo
ataendeleza mapambana zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga,
maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa
maendeleo. Kulia ni mkewe, Profesa Amandina Lihamba.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akishangiliwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Waziri Chikawe ambaye
alijibu maswali ya waandishi wa habari kiufasaha huku akishangiliwa na
wanachama hao, alisema yeye ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na pia
akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo ataendeleza mapambana
zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini pamoja
na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa maendeleo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kulia aliyekaa) akiongoza zoezi la uhakiki wa kadi za
wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuja kumdhamini kugombea
kuteuliwa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, katika
ofisi ya Katibu wa CCM, Wilaya ya Dodoma mjini. Waziri Chikawe wakati
akiwa anajibu maswali ya waandishi wa habari, alisema yeye ni kiongozi
mwenye uzoefu mkubwa na pia akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi
hiyo ataendeleza mapambana zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga,
maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa
maendeleo. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment