Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali.
viti vikiwa tupu baada ya kuahirishwa kwa mdahalo huo.
Mgombea
urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali (kulia),
akizungumza na wadau mbalimbali waliofika kwa lengo la kuwasikiliza
wagombea hao ambao hawakufika.
Mgombea
urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali, akitoka
ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Recency Kilimanjaro baada ya
kuahirishwa kwa Mdahalo wa waliotangaza nia ya kugombea urais kupitia
chama hicho kushindwa kuhudhuria Dar es Salaam juzi. Wagombea hao
walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo ni Mwigulu Nchemba, Samuel Sitta,
January Makamba, Lazaro Nyalandu na Frederick Sumaye.
Na Dotto Mwaibale
WATANGAZA
nia watano wa kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
waliokuwa wahudhurie mdahalo ulioandaliwa na Umoja wa Maofisa Watendaji
Wakuu (CEOrt), walishindwa kuhudhuria mdahalo huo bila ya kuwa na sababu
za msingi ambapo mgombea pekee Amina Salum Ali ndiye aliyejitokeza.
Wagombea
walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo wametajwa kuwa ni Samuel Sitta,
Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye na January Makamba.
Mdahalo
huo ulikuwa uonyeshwe moja moja na Kituo cha Televisheni cha Azam na
Clouds TV ulihudhuriwa na watu mbalimbali na maandalizi yake yalikuwa
yamekamilika.
Kuharishwa
kwa mdahalo huo kuliwasikitisha wadau mbalimbali waliokuwa wamefika
kushiriki wakisema kwamba wagombea hao hawakupaswa kufanya hivyo
ukizingatia kuwa wote ni kutoka chama kimoja cha CCM.
Akizungumzia
kuahirisha mdahalo huo, Mwenyekiti wa Mdahalo huo Ali Mafuruki
hawakupata maelezo yoyote kutoka kwa wagombea ya kuto hudhuria.
Mtangaza
nia pekee aliyefika kwenye mdahalo huo uliokuwa ufanyike ukumbi wa
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, Amina Salum Ali alisema amesitika
sana kwa wenzake kwa kutofika.
Alisema
midahalo kama hiyo ni ya muhimu na ina afya hasa katika wakati huu wa
mchakato wa uchaguzi wa viongozi ambapo wagembea hawapaswa kutukanana
bali kuelewana na kila mmoja wao kuzungumza kile anacho kiamini kwa
maslahi ya taifa.
"Midahalo
kama hii ilikuwa ni fursa kwa watangania kwani wananchi walitaka kujua
tofauti kati ya mgombea huyu au yule lakini ndio hivyo wenzangu
hawajakuja najisikia vibaya" alisema Ali.
Alisema
anashukuru kupata uwanja wa kujiunga na wenzake hasa vijana katika
kinyang'anyiro hicho ingawa amewatangulia kufanya kazi na kuyafahamu
mambo mengi.
Ali
alisema kwamba katika suala la kuinua uchumi haiwezekani kufanya jambo
hilo kwa haraka ni vizuri kwanza vitu vikaweka sawa na kuwe na sera za
kuweza kushawishi kwani hivi sasa kila jambo linakwenda kwa utaratibu.
Alisema
yeye anafahamika sana na amefanyakazi Zanzibar na nje ya nchi na
anauzoefu mkubwa ndio maana akaona anaweza kuongoza taifa iwapo jina
lake litapitishwa kugombea nafasi hiyo.
Alisema
kiongozi anayehitajika ni yule ambaye anaweza kusimamia kwa moyo wa
dhati masuala ya gesi na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo yeye
anaweza kutokana na uzoefu wake kwani anajua sheria na sera.
Watangania
hao walioshindwa kuhudhuria mdahali huo baadhi yao walisema wameshindwa
kufika baada ya kukosa nafasi kutokana na kuwa katika mchakato wa
kwenda mikoani kutafuta wadhamini wa kuwajazia fomu za kugombea nafasi
hiyo na wakaahidi wapo tayari kuhudhuria mdahalo utakaoandaliwa wakati
mwingine. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment