Habari :Waandishi Washauriwa Kuandika Habari Zenye Lengo La Kufichua Changamoto - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 7 November 2022

Habari :Waandishi Washauriwa Kuandika Habari Zenye Lengo La Kufichua Changamoto

Rais ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania( UTPC), Deogratias Nsokolo akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Mkutno Mkuu wa DCPC uliofanyika leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa DCPC, Samson Kamalamo, akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Mkutno Mkuu wa DCPC uliofanyika leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Mawasiliano Tanzania(TCRA),Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Mkutno Mkuu wa DCPC uliofanyika leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Vijana Lumumba, akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa Mkutno Mkuu wa DCPC uliofanyika leo Novemba 6, 2022 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanachama wa  Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam(DCPC) wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Clabu hiyo.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye lengo la kufichua changamoto mbalimbali katika jamii badala ya kuandika habari za kusifia.

Akizungumza leo Novemba 6,2022 wakati wa mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam(DCPC), Rais ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania( UTPC), Deogratias Nsokolo alisema waandishi wamekuwa wakiandika habari za kusifia badala ya kuandika yale yanayowagusa wananchi.

Nsokolo amesema waandishi wanapaswa kukumbuka wajibu wao kwa kuielekeza seriakili matatizo yaliyopo katika sekta za afya, elimu na uchumi.

Amesema serikali imejenga madarasa lakini bado kuna changamoto ya madawati hayatoshelezi, uchache wa walimu wa masomo ya sayansi na kutokuwepo kwa nyumba za walimu.

''Sisi ni sauti ya wasiokuwa na sauti tusiziegemee mamlaka kwani matatizo bado yapo serikali inatekeleza wajibu wake hivyo tunaipenda Serikali yetu tunatakiwa tuieleze changamoto zilizopo kwenye jamii ili zifanyiwe kazi 'mfano kama mkoani Kigoma hatuna meli muda mrefu katika ziwa la Tanganyika,' alisema Nsokolo.

Pia amesema klabu ya DCPC inabeba taswira ya klabu zote nchini hivyo ni muhimu kusuluhisha migogoro ndani ya wanachama wao hivyo inapotokea mtu anayumbisha au anarudisha nyuma klabu husika wachukuliwe hatua haraka.

Naye, Mwenyekiti wa DCPC, Samson Kamalamo, amesema klabu hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vifaa vya ofisi hivyo wamewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia ili waweze kuboresha ofisi yao,

Wakati huo huo Meneja wa Mawasiliano Tanzania(TCRA),Semu Mwakyanjala amesema takwimu za sasa zinaonyesha matumizi ya intaneti yameongezeka kwa asilimia 4,2 kutoka 29,858,759,204 kwa mwaka 2021 hadi kufikia 31,122,163 hadi kufikia septemba mwaka huu.

"Asilimia 95 ya watanzania wapo kwenye maeneo yenye mtandao wenye uwezo wa kutoa huduma za simu za sauti na ujumbe mfupi ambapo asilimia 68 wako kwenye maeneo ya mtandao unawezesha huduma za intaneti ya kiasi 3G na silimia 45 wapo maeneo yenye mtandao wa 4G,"amesema Mwakyanjala.

Mwakyanjala amesema asilimia 90 wamefikiwa na huduma za simu za mkononi ambapo laini za simu zilikuwa 56 milioni mwaka 2021 mpaka sasa laini simu zimefikia 58 milioni kwa mwaka 2022.

Kwa upande wa Meneja wa Mfuko wa Hifadhi wa Jamii kwa Watumishi wa Umma(PSSSF),Rajabu Kinande amesema wanachama wa mfuko huo wanaopata barua ya kibali cha kustaafu kabla ya kustaafu wanatakiwa wafuatilie mapema ili waweze kupata mafao yao kwa wakati.

"Kibali cha kustaafu wanapata miezi sita kabla ya kustaafu ili uweze kufuatilia mapema ili uweze kuanza kulipwa mapema,"amesema Kinande

No comments:

Post a Comment