Matukio : Taswira Mbalimbali za Ziara ya Rais Jakaya Kikwete Nchini Finland na Sweden - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 5 June 2015

Matukio : Taswira Mbalimbali za Ziara ya Rais Jakaya Kikwete Nchini Finland na Sweden


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Spika wa Bunge la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Spika wa Bunge la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi hiyo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akikutana na kufanya mazungumzomna Spika wa Bunge la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi hiyo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mahojiano na wanahabari jijini Helsinki, Finland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtafiti na mwanasayansi  Mtanzania wa mambo ya mawasiliano na mitandao katika Chuo Kikuu cha Aalto cha Helsinki Dkt Edward Mutafungwa alipotembelea chuoni hapo kujionea shughuli za chuo hicho maarufu nchini Finland
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonganisha glasi na Mari Kiviniemi, Waziri wa Masuala ya Nje wa Finland wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa heshima yake jijini Helsinki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mabalozi wa sasa na wa zamani waliopata kuiwakilisha Finland nchini Tanzania
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waishio Finland. Wa pili kushoto ni mwalimu wa Rais Kikwete alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar  es salaam Profesa MarjaLiisa Swantz, ambaye ni Mfini
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyabiashara wa Finland pamoja na washirika wao wa Tanzania baada ya mkutano wao jijini Helsinki, Finland
Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakipata maelezo ya uzaishaji nishati toka kwa viongozi wa kampuni ya Watsila nje kidogo ya jiji la Helsinki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha METSO cha  kutengenezea vipuli vya mitambo ya gesi na mafuta katika jiji la Helsinki, Finland.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Msanii wa Kimataifa wa Kitanzania aishiye Sweden Bw. Charles Njau alipomutana na  Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kipande ambaye mwaka jana alikuwa katika timu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu. Chef Issa, ambaye pia anaedeesha hoteli Mtwara, hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa mkubwa kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio nchii Sweden jijini Helsinki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa 16 wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm, Sweden
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa SIDA Bw. Torbjorn Petterson makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyakazi wa SIDA  katika makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm
Rais Kikwete akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa XVI  wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm
Rais Kikwete akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa XVI wa Sweden

No comments:

Post a Comment