Maisha Yetu : Chef Issa Kipande Akutana na Rais Kikwete nchini Sweden - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 5 June 2015

Maisha Yetu : Chef Issa Kipande Akutana na Rais Kikwete nchini Sweden

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kipande ambaye mwaka jana alikuwa katika timu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu. Chef Issa, ambaye pia anaedesha hoteli Mtwara, hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa mkubwa kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio nchii Sweden jijini Helsinki
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa 16 wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm, Sweden
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa SIDA Bw. Torbjorn Petterson makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyakazi wa SIDA  katika makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm
Rais Kikwete akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa XVI  wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm
Rais Kikwete akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa XVI wa Sweden

No comments:

Post a Comment