Matukio /Kimataifa : Taswira Mbali mbali za Ziara ya Rais Kikwete Nchini Uholanzi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 9 June 2015

Matukio /Kimataifa : Taswira Mbali mbali za Ziara ya Rais Kikwete Nchini Uholanzi

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo na muhtasari wa ziara yake toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi baada ya kuwasili The Hague Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Shell Bw. Ben van Beurden jijini the Hague, Uholanzi Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Bert Koenders jijini The Hague Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katikati wakati Waziri wa Zanzibar Mhe Ramadhani akigonganisha glasi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Mhe. Mark Rutte jijini The Hague  Jumatatu Juni 8, 2015. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mfalme Willem Alexander katika kasri la Kifalme la Noordeinde jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini The Hague Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kuongea na Mabalozi wa nchi mbalimbali za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Uholanzi jijini The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mhe Mark Rutte jijini The Hague Jumatatu Juni 8, 2015. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment