CHAMA
cha Msalaba Mwekundu (Red Cross), Mkoa wa Arusha, kimetoa msaada wa
vyakula, viatu, Blanketi na nguo, kwa wazee nane na watu wenye ulemavu
wa aina mbalimbali 22, ikiwa ni maadhimisho ya chama hicho Duniani,
ambapo kilele chake Mei 8 kila mwaka.
Akizungumza
leo Jijini Arusha, wakati akikabidhi misaada hiyo, Mwenyekiti wa Chama
cha Msalaba mwekundu Mkoa wa Arusha, Christopher Nzera, amesema kuwa
misaada hiyo ni moja ya shughuli zao wanazofanya za kusaidia jamii na
watu wasio na uwezo .
Nzera
ametaja vitu walivyotoa ni pamoja na mchele, nguo za kike na kiume,
sabuni, viatu na fedha kiasi, ili waweze kumudu maisha yao kwa siku
chache.
Aidha amesema katika maadhimisho hayo wameamua kujitolewa uchangiaji
wa damu salama toka kwa wanachama wa chama hicho na kisha itapelekwa
hospitali ya Mkoa Mount Meru Arusha, ili iwasaidie wahitaji wanapopata ajali na majanga mengine.
Amewaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kupenda kujitolea damu kwa ajili
ya kuokoa maisha yaw engine, badala ya kusubiri wakati wwa majanga pekee.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Mkoani Arusha, Phillipo Nery,
ameshukuru msaada huo umefika wakati muafaka, wakati wanaelekea kipindi
cha baridi Mkoa wa Arusha.
Amesema
pamoja na msaada waliopata bado walemavu wanakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo ya ukosefu wa matibabu, licha ya serikali
kuwaahidi kuwapatia bure, lakini kama wazee wameishia kupata vipimo na
kufunguliwa mafaili, ila dawa wanatakiwa kununua wenyewe jambo ambalo
gumu kwao.
No comments:
Post a Comment