WAKATI
Serikali ikionesha kama inatengeneza Mazingira ya Ukiritimba wa
kuvichimbia Kaburi Vyombo vya habari kwa kupitisha Sheria ya Takwimu na
Makosa ya uharifu wa Kimtandao;
Wananchi
wa Kada mbalimbali nchini, na Wadau wa Habari, wanahoji, Rais Jakaya
Kikwete, kusaini Miswada hiyo, anavichimbia Kaburi Vyombo vya Habari na
Waandishi?.
Wana
Zuoni na Waswahili wa Medani za Semi, husikika wakisema, Kwa kawaida,
Ng’ombe, anaweza kutikisa Mkia wake; Lakini kwa dhati, ni agharabu, Mkia
hauwezi kumtikisa Ng’ombe.
Sheria
hizo ambazo zimelalamikiwa na Wadau, kwamba ni Umangimeza wa Kisiasa wa
Watawala, kuvinyanyasa na kuviziba mdomo vyombo vya habari na
Waandishi; Wamesema, kama ilivyokuwa kwa Mordekai; Wanatafsiri Sheria
hiyo itawafunga Mawaziri na Serikali yenyewe.
Katika
nyakati za Utawala wa Mfalme Ahasuero kwenye Biblia Sura ya 7:6-10,
Mordekai alikwenda kwa Mfalme kinyume cha utaratibu, ili kuwanusuru
wananchi waliouzwa ili Waharibiwe, Wauawe, Waangamizwe na kuwa Watumwa
na Wajakazi.
Mbinu
hizo zilipangwa na Akida Mkuu wa Mfalme Ahasuero, Hamani, ambaye
alitaka, Mordekai anayewatetea Wananchi Wasiharibiwe, Wasiuawe,
Wasiangamizwe na kuwa Watumwa na Wajakazi; Atundikwe kwenye Mti,
ukombozi wao usifanikiwe, na watu waendelee kuteseka!. Je iwe hivyo na
kwa Watanzania?.
Hamani
alimwambia mfalme Ahasuero, “Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa
mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme
wako; Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala
hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.
“Basi,
mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa
talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo,
waziweke katika hazina ya mfalme. Ndipo mfalme alipoivua pete yake
mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi”.Esta
3:8-9.
Basi,
Waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya 13 ya mwezi; na barua
zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme,
na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila
jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa
jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake.
Barua
zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme
kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee,
watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya 13 ya mwezi
wa 12 ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara
Nakili
ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa
yote wawe tayari siku ile ile. Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa
amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni.
Mfalme
na Hamani wakaketi ili kunywa divai na kujifurahisha (kama
vile Waziri wa MawasilianoSayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa
akifurahi kusainiwa kwa Miswada hiyo); bali mji wa Shushani
ukafadhaika.
Wadau
wa Habari wanadai, yawezekana hivyo ndivyo Bunge lilivyopelekewa
Miswada ya Sheria ya Takwimu na Makosa ya uharifu wa Kimtandao kwa
kutumia Hati ya Dharula, isainiwe na Rais, ili kuwakomoa Waandishi na
Vyombo vya habari, ikilengwa Uchaguzi Oktoba 2015, ili kuwatisha
Waandishi, Wananchi wasipate nafasi ya kutoa na kupokea habari.
Kama
ulivyotokea uovu wa Hamani kwa Wayahudi, Mordeikai alipojua mambo yote
yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu,
akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.
Mordekai
pia alifika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye
kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia. Na katika kila
jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake iliwasili, palikuwako msiba
mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi
wakalala juu ya gunia na majivu, kama ilivyo kwa Wandishi, Wananchi na
Wadau wake.
Basi
tunaamni, Wananchi wasio na Sauti (Voiceless), ambao vyombo vya habari
ni Mhimili wao wa Nne wa kutetea Kodi na Rasilimali zao, ambao
wamewaibulia Maovu na Machafu Mengi, (Richmond, Dowans, EPA, wa Wanyama
Pori, na hivi karibuni Escrow), watapiga Kelele.
Wanahabari
tunaamini, Kelele zinasikilizwa, na tuna mifano ya kelele kusikilizwa,
‘Migomo ya Wafanya Biashara, Migomo ya Madereva, Wanavyuo, Walimu,
Madaktari na Wauguzi, Wakulima, Wananchi wanaodai Ardhi, Matokeo ya
Uchaguzi ya kughushi, yameiipa Serikali wakati Mgumu.
Mordekai
aliagiza wampelekee Esta jibu la kusema, “Wewe usijidhanie kuwa
utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. Kwa maana wewe
ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na
wokovu kwa njia nyingine; hivyo wanadishi na wadau, msidhani mtaokoka.
“Ila
wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani
ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?tusaidiane
kupiga kelele ya kupinga uovu huu!.
Esta
aliingia kwa Mfalme bila Utaratibu, akakubalika, na akahakikisha badala
ya Mordekai kutundikwa kwenye Mti aliouandaa Hamani, akatundikwa yeye.
Waandishi tushikamane kukataa unyannyaswaji huu wa kutuziba mdomo!
katika
Esta 7:8-10 inasema, Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya
ngome hata mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye
kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema,
‘Namna
gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu?
Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani’.
Ndipo
aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria
mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani
aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo
umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema,
Mtundikeni
juu yake. Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari
Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia; Hivyo pamoja na kwamba Sheria
hizo zimelenga kuwakomoa Waandishi na Vyombo vya habari; Sheria ya
Takwimu kisiasa, zitawafunga Mawaziri.
Kwa
nini nasema na kurudia hayo; kwa sababu watatoa bungeni taarifa za
wizara zisizo sahihi, na itakapofuatiliwa, wataonekana wamesema Uongo.
Chanzo : Vijimambo Blog
No comments:
Post a Comment