Mkurugenzi
wa Global Publishers LTD, Shigongo Eric James (kulia), akishikilia
vitabu vyake baada ya kumpatia jukumu la uzinduzi huo Mhariri Kiongozi
wa Magazeti Pendwa ya Kampuni hiyo, Oscar Ndauka. Tukio hilo limefanyika
mapema leo ndani ya jengo la ofisi za GlobalPublishers zilizoko
Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam.
Meneja
Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia), akiwa
amenyanyua moja ya vitabu hivyo baada ya zoezi la kukata utepe wa
uzinduzi kukamilika. Katikati ni mtunzi wa kitabu hicho, Shigongo Eric
James na Oscar Ndauka, wote wakiwa wamenyanyua vitabu hivyo. Vitabu
vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka
Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to
Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni ’26 Secrets – How to
Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Shigongo
akimkabidhi jukumu la kukata utepe Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa
Oscar Ndauka (wa kwanza kushoto) huku Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo
Abdallah Mrisho anashuhudia zoezi hilo.
Shigongo
akiwaonyesha mojawapo ya vitabu hivyo baadhi ya wanahabari waliokuwa
wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo (hawapo pichani).
Shigongo akiongea machache kwenye uzinduzi huo.
Baadi ya wanahabari kutoka sehemu mbalimbali wakichukua matukio ya uzinduzi huo.
Shigongo akisisitiza jambo juu vitabu hivyo kwenye uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akiwakaribisha wanahabari katika uzinduzi huo.
Afisa
Masoko wa Global Publishers Ltd, Benjamin Mwanambuu, akiongea jambo na
waandishi wa habari kabla ya zoezi la uzinduzi huo kuanza.
Wanahabari wakiwajibika.
Shigongo akisaini moja ya vitabu hivyo tayari ya kukitoa kama zawadi kwa baadhi ya wanahabari walioshuhudia uzinduzi huo.
Mmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo akisainiwa kitabu alichopewa.
Baadhi ya waandishi na wahariri wa Global Publishers Ltd wakisainiwa vitabu hivyo.
Shigongo akisaini kitabu kimojawapo.
MHAMASISHAJI
na mjasiriamali wa kimataifa, Eric James Shigongo, amewaasa Watanzania
kutokata tamaa katika kufuatilia ndoto zao huku wakiamini kuwa wao ni
watu muhimu katika maisha yao na ya jamii.
Akizungumza
na vyombo vya habari mapema leo ndani ya ofisi za Global Publishers
zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar katika uzunduzi maalumu wa vitabu
vyake vitatu, Shigongo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kusoma
vitabu ili kupata maarifa mengi ya juu ya mafanikio maishani.
“Kila mmoja ana ndoto za kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kuondoka mahali alipo.
Wengi
hushindwa kupiga hatua za mafanikio maishani kwa sababu nyingi yakiwemo
mazingira waliyokulia wakiaminishwa kuwa hawawezi kufanya chochote
maishani, jambo ambalo si la kweli kwani kila mmoja anaweza kufikia
ndoto zake akiamua tu kubadili fikra na namna ya kutenda mambo
maishani,” alisema Shigongo.
Vitabu
vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka
Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to
Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni ’26 Secrets – How to
Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Uzinduzi
wa vitabu hivyo ni kuashiria kwake kuingia rasmi mitaani na kusambazwa
kwenye kona mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo vinatarajiwa
kubadilisha maisha ya maelfu ya wasomaji watakaofanikiwa kupata siri za
mafanikio.
(PICHA: MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS/GPL)
No comments:
Post a Comment