Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda ameshinda Tuzo ya Meya Bora
katika Bara la Afrika katika kundi la Majiji ya Kati na kuyabwaga majiji
mengine mbalimbali.
Tuzo
hizo zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (The United
Cities and Local Government of Africa- UCLGA) na kupewa jina la Rais wa
Angola ‘President Jose Eduardo Dos Santos- Africa Mayors Award’ ni za
mara ya kwanza kufanyika Barani Afrika.
Tofauti na Tuzo za Tanzania, Tuzo hizi za Afrika zinahusika na Mamlaka ya miji tu.
Tuzo
hizi zilikuwa ni katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Majiji Makubwa
(Large Size Cities), Tuzo za Majiji ya Kati (Medium Size Cities) na Tuzo
za MajijiMadogo (Small Size Cities).
Tuzo
za Majiji Makubwa (Large Size Cities) zimekwenda jijini Accra, Ghana
wakati zile za Majiji madogo zimechukuliwa na Praia katika visiwa vya
Cape Verde.
Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni ilishiriki mashindano ya Tuzo za Meya
(Halmashauri Bora za Afrika baada ya kushinda Tuzo za Meya/ Halmashauri
Bora Tanzania zilizoandaliwa na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania
(ALAT).
Miradi
iliyoshindanishwa kutoka Manispaa ya Kinondoni ni pamoja na ukusanyaji
wa mapato na kituo cha Mabasi Sinza. Hata hivyo Manispaa ya Kinondoni
ilipimwa katika vigezo vyote vilivyoanishwa na UCLGA.
Zawadi
zilizotolewa ni kikombe, Cheti na Fedha tasilimu kiasi cha Dola za
Kimarekani 100,000 ambazo sawa na shilingi milioni 200.
Majiji
mengine yaliyoshinda yalipata Dola za Kimarekani 200,000 (Sawa na
shilingi Milioni 400) kwa Miji Mikubwa na Dola za Kimarekani 50,000
(sawa na shilingi milioni 100 kwa Miji midogo.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhiwa Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi
la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala
za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana. Mwingine ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Hawa
Ghasia.
Katibu
Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mbando na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty pamoja na
watendaji wengine wakifuatilia kwa makini wakati wa hafla hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Hawa Ghasia akikabidhi cheti cha Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la
Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) kwa Meya wa Manispaa
ya Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyo zilizotolewa na Jumuiya
ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Hawa Ghasia akikabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la
Afrika Kundi la Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na
Jumuiya ya Tawala za Mitaa ya Afrika (UCLGA), kwa Meya wa Manispaa ya
Kinondoni, Yusuph Mwenda katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiwa amenyanyua Tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Hawa Ghasia akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Marekani
100,000 kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda baada ya
kumkabidhi Tuzo ya Meya/ Halmashauri Bora katika Bara la Afrika Kundi la
Majiji ya Kati (Medium Size Cities) zilizotolewa na Jumuiya ya Tawala
za Mitaa ya Afrika (UCLGA) kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment