Rais
wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga akimkaribisha Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges
(kulia) kuzungumza na wakunga nchini waliokusanyika kwenye mdahalo wa
siku moja kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga
Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Musoma mkoani Mara. Kushoto ni
Kaimu Muuguzi mkuu wa serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Ama Kasangala. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Mwandishi wetu, Musoma
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances
Ganges, ametoa wito wa wakunga na wauguzi kubadilisha uzoefu wa shughuli
zao ili kuhakikisha taifa linaondokana na vifo vya wanawake wajawazito
na watoto.
Akizungumza
katika mdahalo kuelekea sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya
wakunga duniani, iliyofanyika kitaifa mkoani Mara, Ganges alisema kwamba
ni wajibu wa wakunga kuhakikisha kwamba dunia ya kesho inakuwa bora na
wanaweza kwa kushirikiana na kubadilishana uzoefu.
Alisema
dunia inawategemea wauguzi kuendeleza kizazi cha binadamu na katika
kufanya hivyo kuna changamoto nyingi zinazotokea changamoto ambazo
zinaweza kumalizwa kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake katika eneo
analofanyia kazi.
Aliutaja wajibu huo kama uongozi, uelimishaji na pia utendaji wa kazi wenye tija na busara.
Alisema nia ya siku ya wakunga ipo wazi ni kuleta ushirikiano kwa ajili ya kuleta dunia iliyo njema ya kesho.
Mtendaji
huyo wa Shirikisho hilo lenye makao makuu yake nchini Uholanzi alisema
kwamba wanafuraha kubwa kusikia mambo makubwa yanayofanywa na wakunga
nchini Tanzania pamoja na changamoto zake zilizopo.
Alisema mafanikio yaliyopo ni matokeo ya ushirikiano na ufanyaji kazi wa pamoja.
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wakunga duniani, Frances Ganges
akizungumza na Wakunga nchini Tanzania waliohudhuria kwenye mdahalo wa
siku moja uliofanyika kwenye ukumbi wa Mara ofisi za Mkuu wa mkoa wa
Mara mjini Musoma kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya siku ya
Wakunga duniani kujadili changamoto zinazowakabili Wakunga nchini.
Katikati ni Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Feddy Mwanga na
Kushoto ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa Serikalim kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk. Ama Kasangala.
Alisema
katika hotuba yake hiyo kwamba wakunga wana wajibu mkubwa wa
kuhakikisha watoto wanazaliwa salama, wanawake wanakuwa salama na kizazi
cha binadamu kinakuwa salama.
Wakati
huo huo Programme Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) Felista Bwana amesema tafiti zilizopo
zinaonesha kuwepo na idadi ndogo ya wakunga wataalamu na kwamba juhudi
lazima zifanyike kuhakikisha kwamba vituo vya afya vyote vina wakunga
wataalamu.
Aidha
mratibu wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy alisema chama
hicho chenye wanachama 3000 miongoni mwa wakunga wauguzi elfu 39
kimelenga kuhakikisha kwamba kila mwanamke mwenye uwezo wa kuzaa anapata
huduma za mkunga mtaalamu .
Alisema kwa sasa ni asilimia 51 tu ya wanawake wazazi wanapata huduma ya wakunga wataalamu.
Alisema ipo haja ya kukubaliana kuwekeza kwa wakunga kwa ajili ya taifa la kesho.
Naye
Daktari bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya wakunga
alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na huduma hafifu.
Aliwataka
wakunga kutumia maarifa zaidi kuokoa maisha ya watoto na wazazi kwa
kuwa na maamuzi ya haraka yanayozingatia uwezo wa eneo analofanyia kazi
na kuhakikisha, kazi zisizowezekana zinapelekwa katika hatua afiki.
Alisema
ipo haja ya mara kwa mara kwa wakunga kuangalia mabadiliko mbalimbali
ya kazi zao kwa kufuatilia wenzao wamefanya nini na sasa tatizo
analoshughulikia wengine wamelifanyaje.
Alisisitiza haja ya ufanyaji maamuzi mapema ili kuokoa maisha ya mtoto na mzazi.
Ofisa
Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges
akisisitiza jambo wakati akiteta na Wakunga nchini ambapo pia aliwatia
moyo kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwataka kuendeleza moyo huo bila
kuchoka.
Alisema
hali hiyo inatokana na ukweli kuwa wazazi wenye uzazi pingamizi
hucheleweshewa kufanyiwa maamuzi na hivyo kuhatarisha maisha ya mtoto na
mzazi.
Wakati
huo huo Rais wa chama cha wakunga nchini (TAMA), Feddy Mwanga alisema
ipo haja ya wakunga kujitathmini na kushirikiana ili kuhakikisha kwamba
huduma wanayoitoa ni ya kiwango cha juu, inayokubalika na kuvutia.
Alisema
wanawake wanapoamua kuzalia kwa wakunga wa kienyeji kuna haja ya
kujiuliza kwanini wanafanya maamuzi hayo wakati vituo vipo na wakunga
wapo.
Alitaka
wakunga kufanyakazi zao kwa bidii na maarifa na kuhakikisha kwamba
huduma zao zinakubalika ili wazazi watumnie huduma zao na hivyo
kuwezesha kuwa na taifa bora.
Aidha
alitaka watumie takwimu vyema katika kuboresha huduma za ukunga katika
maeneo yao na hasa kuhakikisha kwamba zinafikika na zinafanyiwa kazi.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi, Kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
jamii, Rosina Lipyoga akizungumza katika siku hiyo ya mdahalo wa
wakunga ambapo alisema ni aibu kwa watoto na wazazi kufa kutokana na
huduma hafifu.
Programme
Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya
watu (UNFPA), Felista Bwana akitoa mada kwenye mdahalo huo.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya Wakunga nchini waliohudhuria mdahalo huo
wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa
katika mdahalo huo.
Mratibu
wa Chama cha Wakunga nchini (TAMA), Martha Rimoy akielezea umuhimu wa
Wakunga nchini kujiunga na chama hicho pamoja na faida watakazozipata
pindi wawapo wanachama wa TAMA wakati wa mdahalo wa siku moja kuelekea
sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya Wakunga duniani mjini
Musoma.
Kutoka
kushoto ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi
ya watu (UNFPA), Christine Kwayu, Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la
Vyama vya wakunga duniani, Frances Ganges pamoja na Programme Specialist
in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu
(UNFPA), Felista Bwana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa ukumbini hapo.
Msajili
wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Lena Mfalila (kulia) akijumuika
na Wakunga kuimba wimbo wa mshikamano na hamasa mara baada ya
kusikiliza risala fupi ya Ofisa Mtendaji mkuu wa Shirikisho la Vyama vya
wakunga duniani, Frances Ganges (hayupo pichani).
Baadhi ya Wakunda kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki kwenye mdahalo huo wakishiriki kuimba wimbo wa mshikamano.
Programme
Specialist in Health System wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya
watu (UNFPA), Felista Bwana (kushoto) akishiriki kuimba wimbo huo wa
mshikamano.
No comments:
Post a Comment