Meneja Uendelezaji wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara, Abel Yiga,
(kushoto), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Charles Kitwanga wakati waziri huyo alipotembelea maeneo yanayozunguka
mgodi huo ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii
na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za
uchimbaji. Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga,
(Watatu kulia), na kaimu kiongozi wa kitengo cha mahusiano ya kijamii
ya mgodi wa North Mara, Zakayo Kalebo. (kushoto).
Meneja Unedelezaji wa Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya
Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, Asa Mwaipopo, (katikati), akimpatia
maelezo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga,
(kushoto), wakati wa ziara yake ya kutembelea mgodi wa North Mara ili
kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto
ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji.
Kulia ni Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex
Lugendo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (kushoto),
akisalimiana na Meneja Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo,
wakati alipofika kwenye kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na mgodi
wa North Mara, Mara ulioko Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara
Jumatatu Mei 4, 2015, ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi
ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na
shughuli za uchimbaji Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime,
Glorious Luoga,(Watatu kulia), Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi huo, Jimmy
Ijumba, (Wapili kulia) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya
Acacia, Alex Lugendo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, akizungumza na
mama huyu mkazi wa kijiji cha Nyakunguru, kilicho jirani na eeno la
mgodi wa North Mara, huko Nyamongo wilayani Tarime mkoa wa Mara,
wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yanayozunguka mgodi huo
Jumatatu Mei 5, 2015 ili kufahamu jitihada za mgodi kuendeleza miradi
ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi zinapata kutokana na
shughuli za uchimbaji.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, (Wapili kushoto),
akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa nyumba moja
kwa mtindo unaoitwa na wakazi wa Nyamongo "Tegesha", mita chache
kutoka uzio wa mgodi wa North Mara, ili kufahamu jitihada za mgodi
kuendeleza miradi ya kijamii na changamoto ambazo Jamii na Mgodi
zinapata kutokana na shughuli za uchimbaji. Naibu waziri amesikitishwa
na mtindo huo ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la
Nyamongo, hujenga majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo
kwa matarajio ya kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini
iliyofanywa awali.
Meneja wa Uendelezaji wa kampuni ya Acacia, Asa Mwaipopo, (wakwanza
kulia), akiongozana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles
Kitwanga, (wapili kulia), Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya
Acacia, Alex Lugendo, (watatu kulia) na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa
North Mara, unaomilikiwa na Acacia, Jimmy Ijumba, mara baada ya
kukamilisha ziara yake ya kutembelea maeneo yanayozun guka mgodi huo
huko Nyamongo wilayani Tarime Mkoa wa Mara Jumatatu Mei 4, 2015.
Wananchi wakiendelea na ujenzi kwa mtindo wa "Tegesha" mita chache
kutoka eneo la machimbo (pit), la mgodi wa dhahabu wa North Mara, huko
Nyamongo, wilayani Tarime mkoa wa Mara jana. Naibu Waziri wa Nishati
na Madini Charles Kitwanga, amesikitishwa na mtindo huo wa "Tegesha",
ambapo wananchi hususan wanotoka nje ya eneo la Nyamongo, hujenga
majengo haraka haraka eneo la kuzunguka mgodi huo kwa matarajio ya
kujipatia malipo makubwa ya fidia kinyume na tathmini iliyofanywa
awali. Naibu huyo wa waziri yuko ziarani kutembelea maeneo ya mgodi
huo ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment