Baadhi
ya wanahabari mkoa wa Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa mara baada ya kumalizika
kikao chao cha mahusiano mema na kutambulishana kati ya wanahabari na
viongozi wapya wa jeshi la Polisi waliokaa ni kamanda wa polisi
Ramadhan Mungi wa tatu kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard na katibu wa IPC
Francis Godwin na maofisa wengine wa polisi mkoa
|
Baadhi ya askari polisi wakiwa ktk kikao cha pamoja na wanahabari leo
Wanahabari Mkoa wa Iringa wakiwa ktk kikao cha pamoja na maofisa wa jeshi la Polisi
Wanahabari wakiwa katika kikao na jeshi la polisi
|
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akitoa mafunzo mafupi kwa
wanahabari kati ya utendaji kazi wa jeshi la polisi na vyombo vya
habari
|
Na FG BLOG
Wanahabari
wa mkoa wa Iringa leo wamekutana na kamanda wa polisi na maofisa wa
jeshi la polisi Mkoani hapa ili kuendelea kufanya Kazi kwa ushirikiano
kwa faida ya Mkoa wa Iringa.
Katika kikao hicho kilichoambatana na semina fupi ya kukumbushana wajibu wa Kazi za wanahabari na askari.
Akitoa
mafunzo hayo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema
kuwa ili kuufanya Mkoa wa Iringa uweze kufanikiwa ni lazima wabahabari
na polisi kufanya Kazi zao kwa kuzingatia maadili na kutofanya upendeleo
katika utendaji wao.
Mungi
alisema kuwa mbali ya kazi kubwa ambazo vyombo vya habari mkoani hapa
vinafanywa bado jeshi lake limeamua kukutana na wanahabari hao ili
kizidi kuufanya Mkoa kuwa na taswira nzuri ktk mahusiano Kati ya pande
hizo mbili kama njia ya kuwatumikia wananchi.
Alisema
kwa Mkoa wa Iringa vyombo vya habari vimeonyesha mchango mkubwa zaidi
zaidi na kutaka mchango huo na jitihada hizo kuendelea zaidi .
Kamanda
Mungi amesema kuna haja ya wanahabari na askari polisi kuendelea
kujenga mahusiano kwa kukutana na viongozi wao kabla ya kufanya
mapambano yasiyo na tija.
Alisema
kuwa wao kama jeshi la polisi wanatambua kuwa vyombo vya habari ni
muhimu kwa jamii hivyo lazima kujenga mahusiano mema na kuwa askari
polisi hawanasababu ya kuendeleza mivutano
Alisema
kuwa kuna wakati mwingine ajali imetokea na Kazi ya mwanahabari ni
kuhabarisha umma na polisi kuokoa hivyo lazima kufanya Kazi kwa karibu
na kutoa majibu stahiki kwa wanahabari na wanahabari kutotumia jazba
katika utendaji Kazi zao
Akizungumza
katika mafunzo hayo mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa
wa Iringa Frank Leonard alisema kuwa hatua ya jeshi la polisi mkoa
wa Iringa kuandaa kikao hicho cha kufahamiana na mafunzo mafupi kwa
wanahabari ni ya kupongezwa zaidi hasa kwa wakati huu wa kuelekea
katika uchaguzi mkuu .
Alisema
kuwa tofauti baina ya badhi ya askari na wanahabari ilikuwa
ikijitokeza kutokana na pande hizo mbili zinazofanya kazi za kijamii
kutoatambuana vilivyo hivyo kila upande kuonyesha chuki dhidi ya
mwingine jambo ambalo halijengi bali hubomoa.
Leonard
alisema kikao hicho kina umuhimu mkubwa kwa wanahabari hasa wakati
huu wa kuelekea uchaguzi mkuu ambao baadhi ya askari walikuwa
wakiwachukia wanahabari na wanahabari kuwachukia polisi hasa kutokana
na matukio ya nyuma kabla ya Mungi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa huo
wa Iringa.
Katika
hatua nyingine mwenyekiti huyo aliomba jeshi la polisi kuwa na
utaratibu wa kukutana na wanahabari japo kwa mwezi mara moja ili
kujitathimini utendaji kazi wao na pale penye tofauti basi kuweza
kuzimaliza kwa njia sahihi kuliko kila mmoja kutumia nguvu zisizo na
tija.
No comments:
Post a Comment