Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akimpokea Mke wa Rais na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete
wakati alipowasili kwenye uwanja wa mpira wa Shule ya Sekondari
Nyamisati iliyoko wilayani Rufiji kwa helicopter tarehe 2.5.2015. Mama
Salma alikwenda Rufiji kwenye tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa
vijana katika Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama ambayo inamilikiwa na
Taasisi ya WAMA ambapo Mkuu wa Mkoa wa Pwani alikuwa Mgeni Rasmi.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifuatana na Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa
WAMA Mheshimiwa Zakhia Meghji (kushoto) wakiingia kwenye ukumbi wa Shule
ya Sekondari Nwama-Nakayama kuhudhuria Tamasha la Elimu ya Afya ya
Uzazi kwa Vijana wa Shule hiyo tarehe 2.5.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akijumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari
WAMA-Nakayama kucheza wimbo wa ‘Nani ka Mama’ wakati wa Tamasha la Elimu
ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika Shuleni hapo tarehe 2.5.2015.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama wakionyesha maigizo
mbalimbali yanayoweza kumkwamisha mwanafunzi wa kike asifikie malengo
yake wakati wa Tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akitoa mchango wake wa mawzo baada ya kuangalia
maigizo mbalimbali ya wanafunzi wakati wa tamasha hilo.
Baadhi
ya walimu wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa
makini tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana lililofanyika
shuleni hapo tarehe 2.5.2015.
Mtoa
mada kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akieleza umuhimu wa
wanafunzi kufundishwa Stadi za Maisha ili wanafunzi wa kike waweze
kutimiza ndoto zao za maisha.
Baadhi
ya wanafunzi walioshiriki tamasha la siku moja la Elimu ya Afya ya
Uzazi kwa Vijana lililofanyika katika Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama
wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma
Kikwete wakati alipokuwa anatoa salamu zake.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete akimkaribisha
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kutoa hutuba
yake wakati wa tamasha la Elimu ya Afya ya Uzazi kwa Vijana
lililofanyika kwenye Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama na kushirikisha
pia Shule za Mahege na Nyamisati.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akuwahutubia wakati wa Tamasha
la Elimu ya Afya ya Uzazi lililofanyika kwenye Shule ya Sekondari ya
WAMA-Nakayama ikizishirikisha pia Shule za Sekondari Mahege na Nyamisati
tarehe 2.5.2015.
Baadhi
ya wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni
Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo kwenye Tamasha la
Elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana lililofanyika tarehe 2.5.2015 huko
Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko wilayani Rufiji katika Mkoa wa
Pwani.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment