Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya
Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi wakati wa Semina ya Usambazaji wa
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini
Morogoro.
Kamishna
wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said
akitoa maelezo mafupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe akiwahutubia
washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi
ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Baadhi
ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa
makini Semina hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe (katikati) akiwa na
Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu,
Zanzibar na baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro. (
PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)
Na Veronica Kazimoto, Morogoro
Usambazaji
wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni muhimu ili kila
ngazi ya utawala iweze kuzipata, kuzielewa na kuzitumia takwimu
zitokanazo na Sensa hiyo kwa ajili ya kutunga sera, kuandaa na
kutathimini utekelezaji wa mipango ya maendeleo pamoja na kufanya
maamuzi sahihi.
Hayo
yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe
wakati akifungua Semina ya siku moja ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa
ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika mjini Morogoro.
"Ni
matumaini yangu kwamba, ninyi nyote mliokusanyika hapa mtazitumia
vizuri takwimu hizi ili ziwasaidie katika kuweka vipaumbele vya
maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa mkoa wa Morogoro", amesema Dkt.
Rutengwe.
Mkuu
huyo wa Mkoa amesisistiza kuwa ni wajibu wa kila Ofisa wa Serikali
mkoani Morogoro kuhakikisha takwimu zinazotokana na Sensa ya Watu na
Makazi ya mwaka 2012 zinakuwa msingi wa mipango ya maendeleo na kuwa
kigezo cha kufanya maamuzi katika kuweka mstakabali wa mkoa wa Morogoro.
Nae
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo
kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu, amesema lengo la Semina hiyo ni kuwaelimisha wadau
katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri juu ya matumizi ya takwimu
za Sensa ya Watu ili waweze kuzitumia katika kupanga na kutathmini
program mbalimbali za maendeleo katika ngazi husika.
"Dumuni
lingine la Semina hii ni kuhamasisha matumizi ya takwimu rasmi katika
shughuli zetu za kikazi, ili lengo la kutumia takwimu za Sensa kuboresha
maisha ya Mtanzania liweze kutimia", amesema Kwesigabo.
Kwesigabo
amefafanua kua Semina hiyo ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na
Makazi itasaidia kujua ni maeneo yapi mkoa wa Morogoro umepiga hatua na
maeneo ambayo yanapaswa kutiliwa mkazo ili kuweza kufikia malengo ya
kitaifa na kimataifa.
Jumla
ya washiriki mia moja na kumi (110) kutoka ngazi ya Mkoa, Wilaya na
Halmashauri zote mkoani Morogoro wameshiriki katika Semina ya Usambazaji
wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kwa lengo la kupata
elimu juu ya matumizi ya takwimu zinazotokana na Sensa hiyo.
No comments:
Post a Comment