Wanafunzi
wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho,Mariam Rajabu na
Faraja Abdallah wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,
Renatus Rwehikiza (kulia) akiwafafanulia jambo kuhusiana na matumizi ya
kompyuta mpakato zilizokabidhiwa na mfuko huo kwa kushirikiana na
Samsung ikiwa ni msaada kwa wanafunzi wa shule hiyo kuweza kupata
mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta .
Baadhi
ya wanafunzi wa wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho
jijini Dar es Salaam,Juma Hassan, Fadhil Komba na Francis Mwaimbamba
wakijifunza masomo mbalimbali kupitia kompyuta mpakato zilizokabidhiwa
na mfuko huo kwa kushirikiana na Samsung ikiwa ni msaada kwa wanafunzi
wa shule hiyo kuweza kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia
kompyuta.
Mkuu
wa Biashara Endelevu wa Kampuni ya Vodacom Suraya Hamdulay(kushoto)
akifafanuliwa jambo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho
jijini Dar es Salaam, Bernard Yohana, kuhusiana na somo la kompyuta
wakati wa kukabidhiwa rasmi kompyuta hizo pamoja na vifaa vya maabara ya
kompyuta ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Foundation kwa
kushirikiana na Samsung kwa ajili ya kupata mafunzo ya masomo mbalimbali
kupitia kompyuta shuleni hapo.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam, Bernard
Yohana, akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Biashara Endelevu wa Kampuni ya
Vodacom Suraya Hamdulay(kushoto)akimsisitiza jambo kuhusiana na somo la
kompyuta wakati wa kukabidhiwa rasmi kompyuta hizo pamoja na vifaa vya
maabara ya kompyuta ikiwa ni msaada uliotolewa na Vodacom Foundation kwa
kushirikiana na Samsung kwa ajili ya kupata mafunzo ya masomo
mbalimbali kupitia kompyuta shuleni hapo.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya sekondari ya Makumbusho jijini Dar es Salaam
Deogratias Haule, akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu kuhusiana na
kufuata matumizi yaliyo bora ya kompyuta mpakato na vifaa vingine
vilivyokabidhiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung kwa
ajili ya kupata mafunzo ya masomo mbalimbali kupitia kompyuta shuleni
hapo.
Benard
Yohane mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari Makumbusho jijini Dar
es Salaam alionekana kuwa na mshangao wa furaha kwa mara ya kwanza
kusoma somo la bailojia kwa vitendo kwa njia ya kompyuta wakati taasisi
ya Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung ilipotoa msaada wa
kompyuta 25,Screen kubwa ya kufundishia na printer 1 kwa shule hiyo kwa
ajili ya darasa maalumu la kufundishia kompyuta mwishoni mwa wiki.
Wanafunzi
hao wameungana na wenzao wapatao 5000 kutoka shule nyingine za msingi
jijini Dar es Salaam ambao wanapata wanapata elimu ya matumizi ya
kompyuta kwa vitendo na kuweza kujfunza masomo mbalimbali kwa njia ya
mtandao wa internet.Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Samsung
zilizindua mradi huu mwaka 2013 unaojulikana kama Smart na tayari
umeanza kuleta mafanikio kwa kuwawezesha baadhi ya wanafunzi wa shule za
sekondari jijini Dar es Salaam kuingia katika ulimwengu wa sayansi na
teknolojia.Shule ambazo zimenufaika na mradi huu ni
Makumbusho,Kinyerezi,Mtakuja na Kambangwa.
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo,Mkuu wa taasisi ya Vodacom
Foundation Renatus Rwehikiza alisema “ Siku zote tutakuwa mstari wa
mbele kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata elimu bora kupitia
mawasiliano na teknolojia.Mpango huu unawawezesha vijana kupata elimu
bora na kuwaunganisha na wenzao sehemu mbalimbali duniani kote ambapo
wanaweza kupata taarifa mbalimbali na maarifa kwa urahisi.
Alisema
Vodacom inafanya kila jitihada kuhakikisha inaendeleza jamii katika
nyanja mbalimbali kupitia mawasiliano na teknolojia hususani kwa vijana
ambao wanapaswa kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia
ambayo ndiyo yanatawala katika ulimwengu wa sasa wa Sayansi na
Teknolojia.
“Mawasiliano
mazuri huwezesha watu kupata taarifa mbalimbali zinazotokea katika
mazingira yao walipo na sehemu za mbali kwa urahisi.Kwa wanafunzi
kompyuta zinasaidia sana kupata maarifa kupitia mtandao wa
internet.Nawahasa wanafunzi wa Makumbusho msome kwa bidii na mtumie
vizuri fursa hii kutafuta elimu na msiogope kusoma masomo ya sayansi
maana mambo yote hivi sasa yamerahisishwa kupitia teknolojia hii ya
kompyuta”.Alisema.
Mwalimu
Mkuu wa sekondari ya Makumbusho,Bw.Deogratias Haule ameshukuru kwa
msaada huo na kusema kuwa mradi huu ni muhimu na utawawezesha wanafunzi
katika shule yake kuingia katika ulimwengu wa kompyuta na hivi sasa
wanaweza kumudu vizuri somo hilo kwa kuwa wanalisoma kwa nadharia na
vitendo.
Naye
Afisa Mwandamizi anayesimamia shughuli za kijamii kutoka Vodacom
Group,Suraya Hamdulay, alisema mradi wa Smart wa kuwawezesha wanafunzi
kupata elimu kwa njia ya kompyuta ni ukombozi mkubwa na utawawezesha
wanafunzi wengi kutobaki nyuma katika ulimwegu huu wa sayansi na
teknolojia.”Tunaelewa umuhimu wa kuendeleza jamii tunazofanyia kazi ndio
maana leo tumetoa msaada huu kwa shule ya Makumbusho na tuna imani
wanafunzi watafaidika kwa msaada huu na tutafanya jitihada kuhakikisha
wanafunzi wengi zaidi wananufaika”.Alisema.
Akiongea
kwa niaba ya wanafunzi wenzake wenzake Benard Yohane alishukuru kwa
msaada na kusema utawasaidia kujua somo la kompyuta,“Tumekuwa
tukijifunza somo la kompyuta kwa nadharia na kwa kuwa tumepata
kompyuta hivi sasa tutasoma somo hilo kwa vitendo na ndoto yetu ya
kuingia katika ulimwegu wa sayansi na teknolojia imetimia”.
Mwanafunzi
mwingine Subira Suleimani aisema mradi huu ni wa muhimu na unaweza
kuleta mapinduzi makubwa ya kuwawezesha wanafunzi wengi wanaosoma shule
za kawaida hususani zinazomilikiwa na serikali na zilizopo katika
mazingira ya vijijini kuweza kupata elimu kwa njia ya kompyuta na
ktobaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia “Shule nyingi za
serikali hazina kompyuta na nyenzo za kisasa za kufundishia kama zlivyo
shule ningi za binafsi”.Alisema.
No comments:
Post a Comment