Siasa Zetu : Wananchi Mjitokeze kwa Wingi Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura - Natse - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 28 April 2015

Siasa Zetu : Wananchi Mjitokeze kwa Wingi Kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura - Natse


Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira bora karatu mjini jana,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu  la wapiga kura ambayo itawapa  fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika ockoba mwaka huu. (Habari picha na Jamiiblog).

SAM_2311

Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu.
SAM_2293
Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadharakatika uwanja wa mazingira bora karatu mjini
SAM_2292
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kuwapiga chini chama cha mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni jino kwa jino hadi ikulu.
SAM_2279
Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Karatu John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
SAM_2282
Diwani wa kata ya Karatu mjini Jublate Mnyenye aonya Redio mbao zinazosambaza habari kuwa anampango wa kuihama chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)adai yeye na chama hicho ni damu damu.
SAM_2265
Wananchi wakimshangilia Mbunge wao.
SAM_2296
Mzee Peter akijichukulia matukio mbalimbali na simu yake ya mkononi
SAM_2294
Wananchi wa Karatu wakiwa makini kusikiliza
SAM_2304
Mwananchi akieleza kero yake kwa Mbunge wake
SAM_2312
Jackine ambaye aliwakilisha wanawake akiuliza swali kwa Mbunge wake juu ya Hospitali za serikali kukosa dawa. Picha na Pamela Mollel

No comments:

Post a Comment