Mkurugenzi
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Richard Kayombo akitoa neno kuwakaribisha wageni katika
mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Vyuo vya Kodi Afrika uliohudhuriwa na
wajumbe zaidi ya 50 kutoka katika taasisi za kodi barani Afrika, Mkutano
huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na
Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Chuo cha Uongozi wa Kodi Tanzani (ITA) Prof. Isaiah Jairo akiongea
na wajumbe wa mkutano huo na kueleza namna utakavyosaidia katika
kuzijengea uwezo Taasisi za ukusanyaji kodi Afrika hivyo kuweza kuinua
uchumi wa Mataifa mengi ya Afrika.
Mkurugenzi
wa Ujengaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy
Onyonyi akiwaeleza wajumbe wa Mkutano huo namna Kamati hiyo
inavyoshirikiana na Taasisi za Kodi Afrika katika kuzijengea Taasisi
hizo uwezo wa Kiutendaji na kusaidia nchi wanachama kushiriki kuwa na
sera ya pamoja ya masuala ya Kodi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji
kodi.
Naibu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba
Akiongea na wajumbe waliohudhuria Mkutano huo namna Tanzania
ilivyofurahishwa na kuwa mwenyeji wa Mkutano huo wa Kwanza wa wakuu wa
vyuo vya uongozi wa Kodi Afrika na kuwataka wajumbe kutumia fursa hiyo
kujifunza masuala mbalimbali katika sekta hiyo ya ukusanyaji kodi kwani
ni moja ya mhimili muhimu wa maendeleo kwa Mataifa mengi duniani.
Mkurugenzi
Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy
Onyonyi akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika
Nchini Tanzania.
Mkurugenzi
Ujengeaji Uwezo kutoka Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bw. Kennedy
Onyonyi akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo wa kwanza unaofanyika
Nchini Tanzania.
Wakuu wa vyuo vya uongozi wa Kodi Barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment