Mhamasishaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa
katikati akizungumza na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bibi.
Rose Mhina kulia kabla ya kukutana na vijana wa Kata ya Monduli juu na
Kata ya Mfereji kutoa elimu ya ujasiriamali na Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana leo katika Halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha. Kushoto ni Mkuu
wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.
Mhamasishaji
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa
akitoa mada ya Ujasiriamali, Ujuzi na Stadi za Maisha kwa vijana wa Kata
ya Monduli juu na Kata ya Mfereji leo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Monduli Mkoa wa Arusha.
Afisa
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bi. Amina Sanga akiwaelekeza vijana walioudhuria semina ya
Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
kutoka kata za Monduli juu na Mfereji Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
jinsi wanavyotakiwa kuzingatia mwongozo unaosimamia Mfuko wa Maendeleo
ya Vijana.
Mkuu
wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele akitoa mada ya
Uongozi bora wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na
Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri
ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Afisa
Ushirika kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Ester Tarimo
akiteta na vijana wa kata ya Monduli juu na Mfereji namna ya kujiunga na
Saccoss kwa maendeleo ya vijana wakati wa semina ya Ujasiriamali,
Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata
ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Vijana
wa Kata za Monduli juu na Mfereji wakifuatilia kwa makini mafunzo
yaliyokuwa yakitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za
Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo katika Kata ya Monduli juu
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Mmoja
wa washiriki wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana akichangia wakati wa semina hiyo iliyofanyika leo
katika kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa
Arusha.
Vijana
wa Kata za Monduli juu na Mfereji katika picha ya pamoja na
wahamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na
wadau wa vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli baada ya kufunga
semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Kata ya Monduli juu
Halmashauri ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Picha na Genofeva Matemu – Maelezo Monduli.
Na: Genofeva Matemu – Maelezo Monduli
Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kata za Monduli juu na Mfereji wametakiwa kuwa na miradi ya mfano inayokopesheka na inayoonekana ili kuweza kupata fedha zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaosimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Rai hiyo imetolewa na Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa wakati wa Semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika leo katika Kata ya Monduli juu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha.
Bibi. Riwa amesema kuwa jitihada za awali zifanywe na vijana wenyewe kwa kuwa na mwamko wa kuleta maendeleo yatakayotokana na miradi endelevu na yenye malengo kwani kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na hali ya maisha ya sasa na kuwa mfano katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Aidha Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bibi. Rose Mhina amewataka vijana wa Monduli kutokupenda kubebwa kwa kupewa fedha za bure kwa kununuliwa na wanasiasa bali wazidi kujijengea mazoea ya kuwekeza na kuchukua mikopo inayotolewa na Serikali kwa vijana yenye riba nafuu na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili vijana wengine waweze kufikiwa na fursa hiyo.
Akizungumza na vijana wakati wa semina hiyo Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Ester Tarimo amewataka vijana kutokuwa watu wakusukumwa kutafuta maendeleo yao bali wawajibike na kutafuta fursa zilizopo ili kuweza kuondokana na hali ya kutegemea kazi moja ya ufugaji wa mifugo.
“Vijana wa Munduli hamjazaliwa kuishia hapo mlipo, msipende kusukumwa na watu kutafuta maendeleo yenu changamkieni fursa zilizopo na kuwajibika katika jamii zenu bila ya kuwa na ubaguzi wa kijinsia kwani Monduli haitakiwi kuwa kama ilivyo kwa sasa” alisema Bi. Tarimo.
Kwa upande wake mshiriki wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana Bw. Mboyo Kayai amesema kuwa vijana wa Monduli wanaweza kama watapatiwa elimu ya watu wazima kwani kwa sasa jamii kubwa ya vijana katika Halmashauri hiyo hawajui kusoma na kuandika kitu kinachowapelekea kushindwa kuwa na mbinu mbadala za kiujasiriamali.

No comments:
Post a Comment