Afisa
kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) Nicholas
Johanes (wa kwanza kulia aliyechuchumaa aliyeshika simu) akitoa maelezo
kwa kulima(nyuma yake) kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa siku ya
wakulima iliyofanyika katika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga .
Wapili kushoto ni Joseph Mwangono , Afisa kilimo halmashauri ya wilaya
ya Sumbawanga.
Wakulima wakiangalia moja ya shamba darasa Mbeya vijini . Aliyechuchumaa ni Nicholas Johaness, afisa kilimo (ACTN)
Na mwandishi wetu
Mradi
wa kutekeleza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini umekuwa na
mafanikio kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kutumia kilimo
hifadhi lakini changamoto kubwa imeonekana ni ukosefu wa masoko .
Mradi
huo ambao unafadhiliwa na mtandao wa mapinduzi ya kijani barani Afrika
(AGRA )unatekelezwa na mashirika manne katika wilaya sita za mikoa ya
Mbeya na Rukwa katika mazao manne kutokana na eneo husika ambayo ni
Mahindi , mpunga , Soya na maharage kwa kutumia kilimo hifadhi .
Katika
siku ya wakulima iliyofanyika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga ,
Mwenyekiti wa chama cha ushiliki mazao na masoko Laela Amcos Limited
bwana Edom Mwaisemba amesema wakulima wamelima kwa kufuata kanuni bora
za kilimo na kuzalisha mazao mengi lakini kinachowakwamisha ni soko .
‘’ Kwa
mfano mwaka jana tulipata tani 2,500 lakini tukashindwa wapi tutapata
soko . Tunauomba mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN)
kwasababu umetufundisha jinsi ya kulima na tumelima kikamilifu kwa
kufuata kanuni bora na tunaweza kupata hadi tani 3,500 kwa hiyo
tunauomba ututafutie soko’’ alisema bwana Mwaisemba .
Bwana
shamba kutoka taasisi ya kilimo , biashara tegemezi ya mazao mengi ya
mkoani Ruvuma(RUCODIA) bwana Evaresto Joshua amesema kwa kuondoa
changamoto ya soko wamekubaliana na mashirika mengine ya mtandao wa
kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) , CNV na micro finance limited
kuwatumia mawakala wa pembejeo pia kununua mazao .
Changamoto
ya matumizi bora ya mbegu pia imejitokeza katika siku hiyo ya wakulima
ambapo wakala wa mbegu SEEDCO Tanzania Limited imewashauri wakulima
kutotumia mbegu kutoka nje ambazo hazijapimwa na taasisi za ndani ya
nchi .
‘’
Tunajaribu kuwasisitiza wakulima kuhusu matumizi bora ya mbegu bora .
Lakini zaidi tunasisitiza uagizaji na ununuzi wa mbegu ambazo zinatoka
nchi za jirani ziwe zimepimwa na taasisi mbali mbali za nchini mwetu ‘’
alisema bwana Joshua Zuberi , afisa mauzo kutoka wakala wa mbegu
SEEDCO Tanzania Limited .
Nao
wakulima wamesema kilimo hifadhi kimewasidia kuhifadhi udongo na pia
kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji ikilinganishwa na
awali .
‘’
Unakuta mwanzoni heka moja ulikuwa unatumia shilingi 500,000 lakini kwa
sasa hivi angalau inapungua hadi shilingi laki mbili . Unaposema
kupunguza gharama ni sehemu zote kuanzia uandaaji wa shamba . Kwa mfano
kuandaa shamba kunahitaji kutumia moto lakini sasa hivi tunahifadhi
udongo tunafukia mlemle ndani ‘’ alisema bwana Ezebius Chapita , mkulima
kijiji cha Lula .
‘’
Faida nyingine za mradi huu ni kusogeza huduma ya ugani karibu kwa
namna ya kwamba sio kila kijiji kina afisa ugani lakini kutokana na
mafunzo haya ya kilimo hifadhi tumeweza kuwasaidia wakulima viongozi
kutoa taarifa za ugani kwa wakulima wetu na pale inaposhindikana
wanaweza kuwasiliana na sisi kwa kuwasaidia zaidi .’’ alisema Nicholas
Johanes , afisa kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (
ACTN)
Naye
Joseph Mwangono , afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga
ambaye alimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Sumbawanga katika
sherehe hizo alisema kumekuwa na mafanikio kutokana na wakulima
kuzingatia kanuni bora za kilimo
‘’ Kwa
upande wa zao la mahindi wengi sasa wanapanda kwa kutumia mistari
,wanatumia mbolea na wanapalilia kwa wakati tatizo tu linakuwa soko la
zao hilo la mahindi . Kwa zao la maharage zamani walikuwa wanapanda kwa
kumwagilia lakini sasa hivi wanapanda kwa mistari na kutumia mbolea ‘’
alisema bwana Mwangono .
Kanuni
za kufuata katika kutumia kilimo hifadhi ni pamoja na kufunika udongo
kwa kutumia mazao funika au mabaki ya mazao , kutosumbua udongo na
kupanda bila kulima kwa kutumia zana maalum .
Kwa
mujibu wa ACTN , mafanikio ya kwanza katika maeneo maalum Tanzania ni
pamoja kupunguza mmonyoko wa udongo kwa zaidi ya asilimia thelathini .
No comments:
Post a Comment