Nishati Zetu: Ifikapo Machi Mwakani Tatizo la Umeme Jijini Dar es Salaam litakuwa Historia - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Thursday 30 April 2015

Nishati Zetu: Ifikapo Machi Mwakani Tatizo la Umeme Jijini Dar es Salaam litakuwa Historia


 Na Avila Kakingo.
IFIKAPO machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia  kutokana na kukamilika  kwa miundombinu  ya mitambo ya  umeme ifikapo machi mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene katika ziara ya  ukaguzi wa miradi ya umeme ya  Kurasini, Mbagala pamoja na Kinyerezi  jijini Dar es Salaam leo.
Ziara hiyo  iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la  kusogeza miundombinu ya umeme karibu na watumiaji wa umeme.
Simbachawene amesema kuwa  kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa uhakika  inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n amatatizo ya  umeme.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  amesema kuwa matatizo mbalimbali ya  ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi kwa  kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa umeme ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  kuhusiana na uboreshaji wa  Mtambo wa umeme uliopo katika wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  akikagua Mtambo wa umeme uliopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akizungumza na wandishi wa habari katika  Ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa miradi ya umeme jijini Dar es Salaam leo.
 Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo na  Manirabona Emmanuel meneja wa Project wa TANESCO kuhusiana na uboreshaji wa mitambo ya Umeme ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa project wa Tanesco Manirabona Emmanuel akimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  jinsi mitambo ya Umeme itakavyo jengwa katika Mitambo ya Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Mitambo ya umeme ya Mbagala jijini Dar es Salaam. Picha zote na Avila Kakingo.

No comments:

Post a Comment