Meneja
masoko wa benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe kushoto,Meneja masoko
Moshi Eliud Marko katikati wakimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya
sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika kijiji cha kituri
kata ya kileo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro hundi ya shilingi
Milioni tano yenye thamani ya zaidi ya mifuko 300 ya saruji kwaajili ya
ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule hiyo ,msaada huo ni sehemu
ya kamapeni ya Book by Book inayoendeshwa na benki ya CBA ikilenga
kusaidia serikali katika juhudi za Elimu(Picha na Pamela Mollel wa
Jamiiblog)
Meneja
masoko wa Benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe akizungumza na
wanafunzi(hawapo pichani) kuhusu nia yao ya kuwasaidia msaada huo wa
saruji kwaajili ya kujenga hosteli ni kutokana na idadi ya wanafunzi 944
kuwa na changamoto kubwa ya ufaulu hasa jinsia ya kike huku akiwaasa
wanafunzi hao kuwa Elimu ndio urithi pekee wa kuweza kuharakisha
maendeleo Tanzania hivyo jamii inategemea kupata watu muhimu
wakuwasaidia kama madaktari,wafanyakazi wa mabenki na hata walimu wa
kuendeleza elimu
Meneja
masoko Moshi Eliud Marko akiwa anasisitiza wadau mbalimbali wa
makampuni makubwa kujitokeza kusaidia kuinua Elimu ili kupunguza
umaskini Nchini
Mwalimu
mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika
wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa anatoa neno lake la shukrani
kwa Benki ya CBA kwa kufika na kuguswa kusaidia hosteli ya wasichana
katika shule hiyo kutokana na wengi wameshindwa kuendelea na masomo
shuleni baada ya kuingizwa katika mahusiano na wanaume hali ambayo
inawawia vingumu kuweza kumudu masomo.
Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule hiyo Neema Emmanuel akitoa neno la shukrani
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Kifaru wakiwa wanasikiliza kwa makini
Mwalimu
mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa msaada huo alisema Msaada
huo utakuwa kichocheo kwa wanafunzi wa kike kufanya vizuri zaidi ambapo
shilingi Milioni 64 zinahitajika kukamilisha hosteli hiyo itakayoweza
kuhudumia wanafunzi 80
Picha ya Pamoja na Mkurugenzi wa KeyMedia Agency Limited Bi Barbra Lazaro
Mafundi wakiwa wanaendelea na ujenzi wa hosteli ya wasichana shule ya kifaru
Ugeni kutoka Benki ya CBA wakiwa wanashuhudia eneo la ujenzi wa hosteli wakiongozwa na mwalimu Mkuu wa shule hiyo
Kazi inaendelea
Mifuko ya Saruji
No comments:
Post a Comment