Na Ripota Maalum.
Serikali
ya Uingereza imebuni mbinu ya kuwasaidia vijana wa Tanzania katika
kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira kwa kuwapa maarifa na
mikakati ya kujiajiri na kujinadi kwa waajiri .
Vikwazo
vinavyowakabili vijana katika soko la ajira ni pamoja na kutokuwa na
maarifa ya kupata kazi na tabia ambazo zitawawezesha kuwa karibu na
wafanyakazi wenzao,kutoa maamuzi magumu , kutatua matatizo kuweka
heshima na mwisho kuwa wawakilishi bora wa taasisi wanayotumikia .
Kwa
kutambua changamoto hizo Uingereza imetuma walimu wa kujitolea kutoka
taasisi ya Restless Development Organization (ICS)kuwafundisha vijana
mikakati ya kujinasua na matatizo hayo .
Wakizungumza
katika mafunzo waliyoyatoa katika chuo cha Kilimanjaro Institute of
Technology and Management (KITM) walimu hao wa kujitolea wamesema
wanawafundisha vijana namna ya kuandika wasifu wao wenye maelezo ya mtu
binafsi kuhusu elimu, ujuzi na kujiajiri wenyewe .
Kiongozi
wa walimu (ICS) Gemma Bunn aliliambia gazeti hili kwamba sababu ya
kuwapo hapa nchini ni kwa kutambua kuwa Tanzania ina vijana zaidi ya
asilimia 50 ambao hawawezi kupata ajira na wengi hukwama kutokana na
vigezo kama hivyo .
‘’
Tunatoa mafunzo kuhusu maarifa ya kupata ajira ikiwamo namna ya kuandika
maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu , ujuzi , kujiajiri wenyewe na
namna ya kujiweka wakati wa kufanya usaili pamoja na mbinu za kuanzisha
biashara na kujengeneza bajeti ‘’ alisema Bunn.
Mwalimu
Wendy Morrissey anasema wasifu (CV) ni nyaraka muhimu kwa wanafunzi
hivyo ni wajibu kujifunza kuandika . Ni nyaraka itakayowasaidia kupata
ajira na kutaja mambo ya kuyazingatia na kuyaweka kuwa ni pamoja na
ujuzi na maarifa kwa nafasi ya kazi unayoombea .
‘’ CV
haitskiwi iwe ndefu zaidi ya ukurasa mmoja kwasababu mwajiri anachukua
muda wa sekunde nane kuiangalia . Kwa hivyo unatakiwa kumvutia mwajiri
kwa kutumia muda mfupi anapoisoma ‘’
Wakati ukiandika nyaraka hiyo unatakiwa ueleze kwa weledi na usiandike kwa kutumia maneno ya mtaani .
Mambo
mengine ambayo hayatakiwi kuonekana ni sarufi ambazo sio sahihi kwenye
maelezo hayo anawashauri kupitia kwanza maelezo yote pamoja na sarufi
kabla ya kuikabidhi kwa mwajiri .
Jambo lingine la kuepuka ni kuandika maeezo kwa matakwa yao ambayo hayaendani na kazi unayoomba .
Jonathan
Aquilina mmoja wa walimu hao wa kujitolea anayefundisha namna ya
kujiajiri mwenyewe anasema njia rahisi ya kukabiliana na changamoto ya
mikopo ni kujiunga katika vikundi .
‘’
Inaweza kuwa ni kikundi cha marafiki au familia na pale kinapokuwa
kikundi kikubwa hatari inakuwa ndogo . Hiyo ndio njia rahisi ya kupata
mikopo ‘’ anasema Aquilina .
‘’
Njia rahisi ya kujiajiri mwenyewe ni kulifahamu soko lako . Lazima umjue
unaye muuzia bidhaa zako na ufahamu wanahitaji nini . Kama hautafahamu
hautaweza kuuza chechote . Unatakiwa kufanya utafiti wa soko na kufahamu
washindani ni wakina nani na bei wanazouza bidhaa ni zipi ?
Anasema siku zote tathmini biashara yako . Uimara na udhaifu na pia ufahamu kinachoendelea kwenye soko .
Philip
Luke , mratibu wa mafunzo katika chuo cha Kilimanjaro Institute of
Technology and Management ( KITM) wanakofundishwa vijana hao na
mwezeshaji wa mafunzo Dani Kishimbo wanasema mafunzo yamekuwa na umuhimu
mkubwa kwasababu wafanyakazi pamoja na wanafunzi wamepata maarifa mapya
namna ya kuandika wasifu na kuanzisha biashara zao .
‘’
Tumepata maarifa mapya ya namna ya kuanzisha biashara zetu wenyewe na
pia namna ya kujiweka na kujibu maswali wakati wa usaili . Tunafahamu
namna ya kujipanga wakati wa kujibu maswali inavyotakiwa ‘’ anasema Luke
.
Dani
Kishimbo m mratibu wa mafunzo anasema yamekuwa na umuhimu mkubwa na
maarifa waliyoyapata wanafunzi watayatumia kuomba mazoezi kwa vitendo au
ajira .
Taasisi
ya Restless Development mtazamo wao ni kusaidia vijana kuchukua jukumu
la kuwa viongozi kwa kutatua changamoto zinazozikabili chi zao na dunia
kwa ujumla .
Taasisi
hiyo inatekeeza mtazamo huo kwa kuwajengea uwezo vijana kimaarifa ,
kimsukumo na raslimali kuchukua nafasi za kazi ambazo zinachangia sio tu
kupata kipato cha familia bali pia uchumi wa jamii pamoja nan chi zao.
Mafunzo
hayo yamekuja huku kukiwa na ripoti ya Baraza la vyuo vikuu vya Afrika
ya mashariki ikisema karibu nusu ya wahitimu wanaozalishwa na vyuo vya
nchi hizo hawana uzoefu katika soko la ajira .
Ripoti
hiyo inasema wakati maelfu ya vijana wanamaliza kila mwaka , sifa
wanazokuwa nazo haziwezi kuwasaidia kuwapa kazi nawaajiri wanawaacha na
kuchukua wenye ujuzi jambo ambalo linaleta changamoto ya ukosefu wa
ajira katika ukanda huu .
Kwa
mujibu wa katibu wa baraza hilo , profesa Mayunga Nkunya , waajiri
wanasema wahitimu wengi wa vyuo wanakosa kujiamini , hawawezi kujieleza
vizuri na hawana ujuzi wa kitaalam unaotakiwa karika kazi wanazozitafuta
.
No comments:
Post a Comment