Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri,
uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El-
Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Wawekezaji wa Misri wanaotaka kuwekeza katika Sekta ya
Viwanja Wilayani Mkuranga, wakati alipokutana nao kwa mazungumzo leo,
Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri,alikohudhuria mkutano wa
Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa jana Machi 13, 2015 na
Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rais wa Misri, Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi,
wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya mkutano huo, uliofanyika
jana Machi 13, 2015 mjini Sharm El-Sheikh, Misri.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na wageni wake Wawekezaji wa Misri wanaoataka kuwekeza katika
Sekta ya Viwanda Wilayani Mkuranga, baada ya mazungumzo yao
yaliyofanyika leo Machi 14, 2015 mjini Sharm El- Sheikh, Misri
alikohudhuria mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa
jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm
El-Sheikh, Misri. Picha na OMR.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbalimbali wakati
akiwa katika mkutano wa Kiuchumi na maendeleo wa Misri, uliofunguliwa
jana Machi 13, 2015 na Rais wa Misri, Abdel-Fattah El- Sisi, mjini Sharm
El-Sheikh, Misri.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
jana Machi 13, 2015 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa
wa Kiuchumi na Maendeleo nchini Misri. Mkutano huo umeandaliwa na Rais
wa Misri Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi na umehudhuriwa na viongozi
karibu wote kutoka katika nchi za Kiarabu, marais na viongozi wakubwa wa
nchi mbalimbali za Afrika pamoja na wakuu wa vyombo mbalimbali vya
Kimataifa akiwemo pia Waziri wa Mmabo ya Nje wa Marekani John Kerry.
Akizungumza
katika Mkutano huo, Rais wa Misri aliueleza ulimwengu kuwa Misri
imepita jaribio kubwa na sasa iko imara tayari kusonga mbele hivyo wale
wote walio na nia ya kuwekeza nchini Misri wafanye hivyo kwa kuwa
serikali yake itashirikiana nao katika kuwalinda wao na mali zao. Pia
Rais Sisi alifafanua kuwa, nchi yake inarejesha heshima yake iliyokuwa
nayo zamani kutokana na mchango wake katika Umoja wa nchi za Kiarabu
huku pia akisisitiza kuwa Misri sasa inarejea Afrika ambako anatambua
kuna ndugu wa dhati.
Akihutubia
mkutano huo Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal
aliishukuru Misri kwa kuialika Tanzania kuhudhuria mkutano huo na
akafafanua kuwa Tanzania inafurahia uamuzi wa Misri wa kujijenga upya
huku ikikumbuka historia ya kutaka kujiwekea nafasi yake katika Afrika
na katika nchi za Kiarabu.
“Mheshimiwa
Rais, uitishaji wako wa mkutano huu mkubwa ni kiashirio kuwa sasa Misri
inajijenga upya na kwamba inarejesha heshima yake katika Bara la
Afrika, Nchi za Kiarabu na Dunia kwa ujumla,” alisema Mheshimiwa Dkt
Bilal na kuendelea kuwa:
“Tunakupongeza
kwa uongozi thabiti uliouonesha hadi sasa ambapo Misri inaonekana kuwa
imara na thabiti. Uhusiano wetu ni wa kihistoria hivyo Tanzania
inakupongeza na inaahidi kushirikiana nanyi katika ujenzi mpya wa Taifa
lenu.”
Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alitumia nafasi hiyo kuueleza mkutano huo
kuwa eneo ilipo Misri linaunganisha Afrika, Nchi za Kiarabu na Ulaya na
Tanzania nayo iko katika eneo la kitajiri kijiografia ambapo ukiwekeza
nchini Tanzania unakuwa unapata fursa za ziada za kuwekeza katika nchi
za Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika.
“Ukiwekeza
Tanzania utakuwa na uhakika wa soko la watu wasiopungua milioni 400 na
nchi zetu ni lango la nchi zipatazo nane ambazo hazina bahari,”
mheshimiwa Makamu wa Rais alisema na kufafanua kuwa Tanzania
inakaribisha wawekezaji kama ambavyo Misri inafanya na zaidi akaeleza
kuwa fursa za uwekezaji Tanzania ni nyingi na hasa sasa ambapo
tunaelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Katika
mkutano huu, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata nafasi ya kukutana na
Mheshimiwa Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi na kuzungumza naye na
kisha kuhudhuria mada ya kiuchumi iliyowasilishwa na Waziri Mkuu wa
Misri Ibrahim Mahlab. Mheshimiwa Makamu wa Rais na msafara wake
wanarejea nyumbani kesho tayari kuendelea na majukumu mengine ya
Kitaifa.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Sharm el Sheikh, Machi 14, 2015
No comments:
Post a Comment