Ajali Dodoma : Basi la Osaka Lapinduka Baada ya Kuligonga tela la Lori ,Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 14 March 2015

Ajali Dodoma : Basi la Osaka Lapinduka Baada ya Kuligonga tela la Lori ,Dodoma


Basi lenye namba za usajili T. 197 Scania mali ya kampuni ya OSAKA likiwa limepinduka baada ya kugonga tela lililokuwa limeharibika njiani.
Mnamo tarehe 13/03/2015 majira ya saa 23:34hrs huko barabara kuu ya Diodoma/Morogoro eneo la Chuo cha Biashara (CBE) Kata ya Makole Manispaa ya Dodoma kwenye makutano ya barabara maarufu kama kona ya Dodoma Inn, gari lenye namba za usajili T. 197 BUS Scania bus mali ya kampuni ya OSAKA likiwa na abiria 57 likiendeshwa na Dereva SAID CHAUPENDO MSHANA mwenye miaka 33, Mkazi wa Dar es Salaam likitokea Bukoba kwenda Dar es Salaam, liligonga tela lenye namba za usajili T. 533 BNM la gari lenye namba za usajili T. 426 BMJ Scania lililokuwa likiendeshwa na IDD JUMA mwenye miaka 41, Mkazi wa Njedengwa Manspaa ya Dodoma lililokuwalimeharibika.


Basi la OSAKA baada ya kushusha abiria stendi kuu ya mabasi Dodoma liliondoka stendi likiwa katika mwendokasi na kushindwa kusimama pamoja na kusimamishwa na Askari wa usalama barabarani waliokuwa kwenye eneo ambalo tela lilipoharibikia. Kutokana na mwendokasi  aliligonga  tela kisha kutumbukia mtaroni pembeni mwa barabara katika uzio wa chuo cha Biashara (CBE) na kusababisha majeruhi kwa abiria mmoja aliyefahamika kwa jina la JUSTA TRAZIAS mwenye miaka 19, Mkazi wa Ubungo River side Dare es Salaam ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa Dodoma kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri. Dereva wa basi hilo amekamatwa na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta kondakta wa basi hilo.

 Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva, mwendokasi na kukataa kutii amri ya Askari aliposimamishwa kisha kushindwa kulimudu gari na kusababisha ajali hiyo.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ametoa wito kwa madereva kuwa na udereva wa kujihami na wenye kuchukua tahadhari. Pia abiria waone umuhimu wa kutoa taarifa pale wanapoona dereva anaendesha mwendokasi na kutotii sharia za usalama barabarani mfano dreva huyu pamoja na kuwa mwendokasi pia  inaonyesha alikuwa anakiuka maelekezo ya mabasi kutotembea baada ya saa sita usiku kwani kwa muda huo alitakiwa walale stendi ya mabasi Dodoma na ndiyo maana aliposimamishwa na Askaria likataa kusimama na matokeo yake akasababisha ajali hii.

No comments:

Post a Comment