Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa
(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa
akimfafanulia jambo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa
jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus
Nkwela ( aliyesimama) akifafanua jambo mgeni rasmi Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) wakati hafla ya
uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo
Mikocheni jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.Kulia ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati)akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi(NACTE) kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa (NACTE)
Dkt. Primus Nkwela,Kamishina wa Elimu Profesa Uestella Bhalalusesa,Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara wa wizara hiyo Consolata Mgimba na Mwenyekiti wa
barabaza la Taifa la Elimu ya Ufundi Mhandisi Steven Mlote.Hafla hiyo
ya Uzinduzi ilifanyika katika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba wakizinduzi jengo jipya la
Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uzinduzi huo
ulifanyika makao makuu ya NACTE Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
Katibu
Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sifuni Mchome
akinongonezwa jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo
jipya la Mitihani uliofanyika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) na
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus
Nkwela wakati alipokuwa akisoma lisala wakati wa hafla ya uzinduzi wa
jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)
uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus
Nkwela, akisikilizwa jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na wadau wengine wa elimu wakati
alipokuwa akielezea jinsi walivyofanikiwa kujenga jengo hilo jengo hilo
wakati wa uzinduzi wa jengo hilo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati)
akimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi
Steven Mlote baada ya kumkabidhi zawadi katika hafla ya uzinduzi wa
jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)
uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akionesha cheti
halali cha matumizi ya jengo jipya alilolizindua la Mitihani la Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) lililopo makao makuu ya Baraza hilo
Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
Wakishuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela
na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven
Mlote.
Katibu
Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sifuni Mchome( kulia)
akisikilizwa kwa makini na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dkt.Shukuru Kawambwa (kushoto ) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela (katikati)alipokuwa
akifafanulia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la
Mitihani lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Serikali imesema itaendelea kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha ili kuliwezesha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutekeleza malengo yake ya kukuza stadi na maarifa kwa idadi kubwa ya vijana wanaohitimu shule za msingi na za sekondari.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la mitihani la baraza hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa alisema sekta ya elimu hususani Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi inakuwa kwa kasi kubwa haswa ikizingatiwa kuwa wahitimu wa ngazi za elimu ya msingi na sekondari inaongezeka kila mwaka.
Waziri Kawambwa alieleza kuwa, wahitimu wengi hawapati fursa za kuendelea na masomo hadi ngazi ya vyuo vikuu. “Wahitimu hawa wanahitaji fursa mbali mbali za kukuza stadi na maarifa ambazo zitawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha yao ya kila siku na kuingi katika soko la ushindani la ajira ndani nan je ya nchi,” alielezaa
Kuhusu ongezeko la vyuo vinavyoendesha mafunzo ya Ufundi alisema inaonyesha kuwa hadi sasa kuna idadi ya vyuo takribani 501 na kozi zipatazo 1050 kuanzia ngazi ya Cheti hadi Shahada ya kwanza zinazoendeshwa katika vyuo kwa udhibiti wa Baraza.
“Huu ni ushahidi tosha kuwa mahitaji ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa vijana wetu ni makubwa ukilinganisaha na uwezo wetu wa kutoa mafunzo hayo. Hivyo, ipo haja kwa baraza kuimarisha Ofisi za kanda ili ziweze kutoa huduma za karibu, kwa wakati na kwa grarama nafuu,” alieleza
Kwa upande wake mwenyekiti wa Braza hilo Injinia Steven Mlote alisema ili kuhakikisha vyuo vinazingatia masharti ya usajili wao na vinatoa elimu bora, Baraza limeweka nguvu kubwa katika kufuatilia na kusimamia ubora wa elimu unatolewa na vyuo vilivyosajiliwa na baraza
“Baraza limefungua ofisi katika kanda 6 kwa ajili ya kusogeza huduma mikoani na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji. Aidha, kukamilika kwa jengo hili ni utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha huduma za kudhibiti ubora kwa vyuo na uendeshaji mitihani ulioanza kwa kununua mitambo ya kuchapisha mitihani,”
Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alisema kuwa kutumia Sheria na Kanuni zake, Baraza limetoa notisi ya siku 30 kwa vyuo na taasisi 13 kufungiwa na kufutiwa usajili endapo havitakidhi vigezo vya baraza na pia aliatangaza kutolewa kwa notisi ya kuvishusha hadhi vyuo na taasisi 61.

No comments:
Post a Comment