Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga
Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyekwemnda kumuomba udhuru ili kuondoka
mapema kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Jaji
Geoffrey W. M. Kiryabwire akiongozwa kuelekea jukwaani kula kiapo kuwa
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimpongeza Jaji Audace Ngiye kutoka Burundi baada ya kula kiapo kuwa
Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 16
wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimpongeza Mhe Liberag Mpfumukeko kutoka Burundi baada ya kuteuliwa
kuwa Nibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki wakati wa mkutano
wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Waziri
wa Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia
ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Dkt Harrison
Mwakyembe akishauriana jambo na KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Joyce Mapunjo wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Wanafunzi
washindi wa Insha wakisubiri kupokea tuzo zao katika mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais
Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akipungia mkono wajumbe walioko Kampala
baada ya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kuzindua mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya moja kwa moja
kwa njia ya video uitwao Telepresence katika mkutano wa 16 wa kawaida
wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Ujumbe
wa Tanzania katika mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika
Mashariki February 20, 2015, Kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nchi
za Nje Mhe Bernard Membe, WAZIRI wa nchi ofisi ya rais anayeshughulikian utawala bora Mhe. George Huruma Mkuchika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Mcheche Masaju, Waziri wa Fedha, Mhe, Saada Mkuya Salum na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia katika kilele cha mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya na Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini baada ya mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi
jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa
wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi
za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwindikiza na Rais Pierre Nkurunzinza wa
Burundi walipokutana jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakipigiwa wimbo wa taifa wa
Tanzania baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za
Afrika Mashariki February 20, 2015. Kulia ni Naibu Rais wa kenya Mhe. William Samoei Ruto
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakisimama kwa wimbo wa mataifa ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu
wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakiwa meza kuu kwenye ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa mkutano wa
16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongoza mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
February 20, 2015
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana
mikono na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kupokea kijiti cha
kuongoza jumuiya hiyo wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Waziri
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa
baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Dkt Harrison Mwakyembe akiwasilisha
ripoti ya mwaka ya baraza hilo mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Bango la wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya
baada ya kukabidhiwa ripoti ya mwaka ya baraza hilo mkutano wa 16 wa
kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti
mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na
Rais Uhuru Kenyatta wa kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na
Naibu Rais wa kenya Mhe. William Samoei Ruto baada ya mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015. Picha zote na IKULU
No comments:
Post a Comment